Rais wa Malawi aelezea kilichomfanya kushindwa kutengeneza ajira milioni moja,

October 6, 2020

Rais Lazarus Chakwera alichaguliwa tena katika uchaguzi uliorudiwaImage caption: Rais Lazarus Chakwera alichaguliwa tena katika uchaguzi uliorudiwa

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameangazia ahadi yake aliotoa wakati wa kampeni ya kutengeneza ajira milioni moja na kusema kwamba serikali inaweza tu kutengeneza ajira 200,000.

Rais Chakwera alisema serikali haikuweza kutimiza ahadi peke yake na kuwa ilihitajika usaidizi kutoka kwa sekta za kibinafsi.

Alisema kwamba kila mjasiriamali alihitajika kuajiri watu wengi zaidi.

Rais alisema hayo wakati wa kusherehekea siku 100 tangu serikali yake ilipoingia madarakani hapo Jumatatu.

Ahadi ya kutengeneza ajira milioni moja ndio ilikuwa gumzo kwa Muungano wa Tonse uliochaguliwa katika uchaguzi wa urais uliorejelewa.

Wakosoaji wake wameambia vyombo vya habari kwamba muungano huo haukuwa na mpango wa kutengeneza ajira na ulikuwa tu unautumia kama mkakati wa kampeni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *