Rais wa Iran alaani mataifa ya Ghuba kwa kurejesha uhusiano na Israel, on September 16, 2020 at 6:00 pm

September 16, 2020

 Rais wa Iran Hassan Rouhani amezikosoa Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kurejesha uhusiano na Israel. Rouhani amezitaja nchi hizo kama watumwa wa Marekani ambao viongozi wao wanatishia usalama wa ukanda mzima wa Mashariki ya kati. Matamshi yake haya aliyoyatoa kupitia taarifa yanakuja baada ya UAE na Bahrain kutia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel hapo jana. Tukio hili lilifanyika katika ikulu ya White House mbele ya Rais Donald Trump. Kwa sasa kuna jumla ya nchi nne za Kiarabu ambazo zina uhusiano wa kidplomasia na Israel zikiwemo Misri na Jordan.,

 

Rais wa Iran Hassan Rouhani amezikosoa Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kurejesha uhusiano na Israel. 

Rouhani amezitaja nchi hizo kama watumwa wa Marekani ambao viongozi wao wanatishia usalama wa ukanda mzima wa Mashariki ya kati. 

Matamshi yake haya aliyoyatoa kupitia taarifa yanakuja baada ya UAE na Bahrain kutia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Israel hapo jana. 

Tukio hili lilifanyika katika ikulu ya White House mbele ya Rais Donald Trump. 

Kwa sasa kuna jumla ya nchi nne za Kiarabu ambazo zina uhusiano wa kidplomasia na Israel zikiwemo Misri na Jordan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *