Rais wa Burundi azuru Tanzania kwa mara ya kwanza

September 19, 2020

Dakika 4 zilizopita

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

Maelezo ya picha,

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye akiwa na mwenzake wa Tanzania John Magufuli

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya siku moja kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli.

Bwana Ndayishimiye amewasili katika uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma asubuhi ya Juamosi na kupokelewana mwenyeji wake rais Magufuli.

Ziara hii ni ya kwanza rasmi kwa rais Evariste Ndayishimiye kuitembelea Tanzania tangu kuingia kwake madarakani.

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

Maelezo ya picha,

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kutiwa saini na Mkurugenzi wa mawasiliano ya serikali Emmanuel Buhuhela, bwana Ndayishimiye na mwenyeji wake ”watazungumza na Watanzania katika uwanja wa Lake Tanganyika kabla ya kuzindua jengo la mahakama Kuu ya Tanzania, Kigima na baadae kuwa na mazungumzo rasmi katika Ikulu ndogo-Kigoma”

Burundi na Tanzania zimekuwa na uhusiano wa karibu kutokana matukio kadhaa ikiwemo ya hivi karibuni ambapo Tanzania ilikuwa nchi pekee iloyotuma wajumbe wake wake kwenye mazishi ya rais wa zamaniwa Burundi Pierre Nkurunziza na kuapishwa kwa Ndiyashimiye.

Burundi kwa upande wake ilijibu fadhila hiyo kwa kumtuma Waziri Mkuu wao kwenye mazishi ya rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, JOHN BUKUKU-KIGOMA Maelezo ya picha, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye akiwa na mwenzake wa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *