Rais wa Belarus aliweka jeshi katika tahadhari

September 18, 2020

Rais wa Belarus anayekabiliwa na mbinyo Alexander Lukashenko ametangaza kuwa ameliweka jeshi katika tahadhari kubwa na kufunga mipaka ya nchi hiyo na Poland na Lithuania. Uamuzi wa Lukashenko unatilia mkazo madai yake ya kila mara kuwa wimbi la maandamano dhidi yake linachochewa na nchi za Magharibi. Anakabiliwa na ukosoaji kutoka kwa Marekani na Umoja wa Ulaya. Lukashenkoamesema anawaondoa wanajeshi mitaani na kuwapeleka mipakani ili kuimarisha ulinzi hasa katika mpaka na Ukraine “Sitaki nchi yangu kuwa vitani. Isitoshe, sitaki Belarus na Poland na Lithuania kugeuka kuwa maonyesho ya kijeshi ambako masuala yetu hayatatuliwa. Kwa hivyo, leo mbele ya watu hawa wazuri kabisa, na wazalendo ninawaomba watu wa Lithuania, Poland na Ukraine – kuwakomesha wanasiasa wenu vichaa, msiruhusu vita izuke.” Soma pia: Lukashenko yuko Urusi kwa mazungumzo na Putin

Maafisa wa Poland wamesema hali bado haijabadilika mpakani. Pawel Jablonski amesema wanaichukulia hatua hiyo ya Lukashenko kuwa mchezo wa kisaikolojia ambao unalenga kutengeneza picha ya kitisho cha nje.

Maafisa wa mpakani wa Lithuania pia wamethibitisha kuwa hali katika mpaka na Belarus bado ni ya kawaida, wakisema wanasubiri kuona jinsi mabadiliko hayo yatavyotekelezwa.

ARCHIV Sotschi Lukaschenko und Putin (Reuters/S. Chirikov)

Urusi ndio muungaji mkono mkubwa wa Lukashenko

Mapema jana, mgombea mkuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais ambao matokeo yake yalipingwa Sviatlana Tsikhanouskaya alisema wanaharakati wanatayarisha orodha ya polisi wanaodaiwa kuhusika katika ukandamizaji dhidi ya waandamanaji.

Hapo jana, bunge la Ulaya lilipitisha kwa wingi azimio linalopinga matokeo rasmi ya uchaguzi na kusema halitamtambua Lukashenko kuwa rais halali mara baada ya muhula wake utakamilika Novemba 5. Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi ilijibu ikisema wamesikitishwa kuwa Bunge la Ulaya, ambalo linajiweka kuwa mpiganiaji wa demokrasia, limeshindwa kupata nia ya kisiasa na kuangalia picha pana zaidi, na kutopendelea upande mmoja. Soma pia: Putin kuipa Belarus mkopo wa dola bilioni 1.5

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki amesema leo wakati wa ziara yake nchini Lithuania kuwa nchi hizo mbili ambazo ni majirani wa Belarus, zitaendelea kutoa msaada wa matibabu na vifaa kwa Wabelarus walioumia na kuteswa wakati wa maandamano.

Karibu nchi 30, zimetoa taarifa ya mapema leo zikiitaka serikali ya Belarus kurejesha huduma za intanet, mbinu inayotumiwa mara nyingi na serikali kandamizi kuuzuia upinzani kufanya harakati zao.

Wakati huo huo, Shirika la Usalama na Ushirikiano Ulaya – OSCElenye nchi 17 wanachama limezindua uchunguzi kuhusu ukiukaji wa haki likisema nia ni kuwawajibisha maafisa wa Belarus.

afpe, ap, reuters, dpa
https://www.dw.com/en/belarus-president-puts-military-on-alert-amid-eu-border-tensions/a-54970561

Source link

,Rais wa Belarus anayekabiliwa na mbinyo Alexander Lukashenko ametangaza kuwa ameliweka jeshi katika tahadhari kubwa na kufunga mipaka ya nchi…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *