Rais wa Afghanistan ateuwa kundi la upatanisho kwa mazungumzo ya amani, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 3:00 pm

August 30, 2020

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ametangaza wajumbe na uongozi ulioteuliwa wa baraza kuu la maridhiano ya kitaifa nchini humo katika juhudi za kusukuma mbele mazungumzo ya amani.Agizo la rais lililotolewa hapo jana jioni, limesema kuwa lengo la uteuzi wa wanasiasa hao wa kiwango cha kitaifa lilikuwa kutafuta makubaliano ya kitaifa ya kuongoza mazungumzo hayo ya amani. Wanasiasa wa ngazi za juu, viongozi wa vyama vya kisiasa na viongozi maarufu wa kidini ni miongoni mwa wanachama wa baraza hilo.Agizo hilo la rais lililipa baraza hilo kuu jukumu la kuunda mkutano mkuu wa baraza hilo katika muda wa wiki moja kwa kuhusisha watu wa matabaka mbali mbali nchini humo.Ni mwanamke mmoja pekee aliyeteuliwa katika baraza hilo kuu ambalo pia lilikosa uwakilishi wa vijana hali iliyoibua shtuma kali.Baraza hilo kuu la maridhiano ya kitaifa ni taasisi tofauti inayosimamia kundi la wanachama 21 wa mazungumzo ya amani lililoundwa ili kuwezesha mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la Taliban.,

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani ametangaza wajumbe na uongozi ulioteuliwa wa baraza kuu la maridhiano ya kitaifa nchini humo katika juhudi za kusukuma mbele mazungumzo ya amani.

Agizo la rais lililotolewa hapo jana jioni, limesema kuwa lengo la uteuzi wa wanasiasa hao wa kiwango cha kitaifa lilikuwa kutafuta makubaliano ya kitaifa ya kuongoza mazungumzo hayo ya amani. Wanasiasa wa ngazi za juu, viongozi wa vyama vya kisiasa na viongozi maarufu wa kidini ni miongoni mwa wanachama wa baraza hilo.

Agizo hilo la rais lililipa baraza hilo kuu jukumu la kuunda mkutano mkuu wa baraza hilo katika muda wa wiki moja kwa kuhusisha watu wa matabaka mbali mbali nchini humo.

Ni mwanamke mmoja pekee aliyeteuliwa katika baraza hilo kuu ambalo pia lilikosa uwakilishi wa vijana hali iliyoibua shtuma kali.Baraza hilo kuu la maridhiano ya kitaifa ni taasisi tofauti inayosimamia kundi la wanachama 21 wa mazungumzo ya amani lililoundwa ili kuwezesha mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la Taliban.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *