Rais Trump na Mke Wake Waambukizwa Virusi vya Corona

October 2, 2020

Rais wa Marekani, Donald Trump, na mkewe Melania Trump, wamepata maambukizi ya virusi vya corona. Rais Trump, muda mfupi uliopita ameandika kupitia ujumbe wa Twitter kwamba, yeye na mke wake wameambukizwa Covid-19. Kupitia ujumbe huo, rais Trump amesema kwamba atajiweka kwenye karantini kwa siku 14, kama inavyo elekezwa na wataalamu wa afya. Taarifa hiyo ya kuambukizwa Covid-19

imethiitishwa na vituo mbalimbali televisheni vya Marekani. Daktari wa White House, Ronny Jackson, amethibitisha juu ya taarifa hizi, lakini ameeleza kwamba rais Trump, na mke wake wapo katika hali njema. Imeelezwa kuwa rais ataendelea na majukumu yake wakati anafuata taratibu za kiafya. Kabla ya ujumbe wa Twitter, wa rais Trump, kutangaza kuambukizwa Covid-19, alitangaza kwamba mkurugezi wa mawasiliano wa White House, Hope Hicks, ameambikizwa Covid-19. Katika ujumbe wake, rais Trump, amewema “watapamabana na ugonjwa huo na watakuwa salama.” Tutawaletea taarifa zaidi kadri tutakavyo zipata.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *