Rais Trump, arejea ofisini Jumatano

October 8, 2020

Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye amekutwa na maambukizi ya Covid-19, alirejea katika ofisi ya rais ndani ya White House, Jumatano mchana.

Hii ilikuwa ni mara ya kwanza toka aruhusiwe kutoka hospitali siku mbili zilizopita baada ya kuambukizwa virusi vya corona.

Rais alitembea kutoka katika makazi yake mpaka kwenye ofisi yake kwa ajili ya kupatiwa muhtasari wa mazungumzo ya muswada wa kutoa fedha za afueni kwa raia wa Marekani, na kimbunga Delta, kwa mujibu wa maafisa wa White House.

RaisTrump, aliandika ujumbe wa Twitter, muda mfupi baadaye kueleza kwamba ameelezwa kuhusu kimbunga, na amezungumzia masuala ya maandalizi na magavana wa Texas, na Lousiana.

Msemaji wa White House, Brian Morgenstern, amesema kwamba rais anataka kuzungumza na watu wa Marekani mapema, lakini hilo bado halijaamuliwa.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *