Rais Trump apuuzilia mbali virusi vya corona baada ya kutoka hospitali

October 6, 2020

Dakika 3 zilizopita

virusi vya corona
Maelezo ya picha,

rais Trump apuuzilia mbali

Rais wa Marekani Donald Trump amerejea kwa kishindo katika Ikulu ya White House kuendelea na tiba ya virusi vya corona baada ya kulazwa hospitali kwa siku tatu.

Rais alitoa barakoa yake katoka roshani ya White House, ambako wafanyakazi kadhaa na washauri wake walipatikana na virusi hivi karibuni.

“Najihisi vyema sana!” Bw. Trump awali aliandika katika Twitter yake.”Usiogope Covid. Usiache itawale maisha yako.”

Zaidi ya watu milioni 7.4 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Covid-19 nchini Marekani. Virusi vya ugonjwa huo vimewaua takriban Wamarekani 210,000.

Maswali bado yanaibuliwa kuhusu ugonjwa wa Bw. Trump baada taarifa kinzani kutolewa wikendi iliyopoti kuhusu hali yake. Ukubwa wa mlipuko wa virusi katika Ikulu ya White House bado unaendelea kuwa kitendawili.

Nini kilifanyika Trump alipotoka hospitali?

Akiwa amevalia suti , tai na barakoa, Bw.Trump alitoka nje ya Hospitali ya kitaifa ya kijeshi ya Walter Reed mjini Washington DC Jumatatu usiku akikunja ngumi na kuinua mkono juu.

Asanteni sana,” alisema, akipuuza maswali kutoka kwa wanahabari, akiwemo mmoja aliyemuuliza: “Una uhakika hutasambaza virusi bila kujua bwana Rais?”

Baada ya safari fupi ya helikopta, Bw.Trump alipigwa picha akiwa peke yake kwenye roshani ya Truman katika Ikulu ya White House. Alivua barakoa, kisha akainua juu kidole gumba na baadae kupiga saluti ya mtindo wa kijeshi.

Saa chache baadae, aliweka ujumbe kwenye Twitter kama ishara kwamba anajiandaa kurejea kwenye msururu wa kampeni.

Muda mfupi kabla ya kuondoka hospitali, aliandika ujumbe kwenye Twitter yake na kusema: “Nitarudi kwe kampeni hivi karibuni!!! Taarifa feki zinaonesha kura feki za maoni.”

Bw.Trump anagombea muhula wa pili madarakani na atakabiliana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden chini ya mwezi mmoja katika uchaguzi mkuu wa urais.

Akiwahusia Wamarekani wasiogope ugonjwa wa corona katika ujumbe wake wa awali kwenye Twitter siku ya Jumatatu, Bw. Trump aliongezea kusema: “Utawala wa Trump, umetengeza dawa na kujifunza mengi. Najihisi vyema zaidi kuliko miaka 20 iliyopita!!”

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, madaktari wa rais hawakutoa maelezo zaidi kuhusu tiba yake, walisema anaendelea vyema na kwamba atapewa dozi nyingine ya dawa ya remdesivir kabla ya kuruhusiwa kuondoka hospitali.

madaktari wa Trump wasema rais huyo yuko shwari
Maelezo ya picha,

madaktari wa Trump wasema rais huyo yuko shwari

Kutolewa kwa rais hospitali kunakuja wakati ambapo visa zaidi vya maambukizi vimeripotiwa miongoni mwa wafanyakazi wa White House.

Karibu maafisa 12 wa ngazi ya juu waliotangamana na rais Trump wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona, wakiwamo pia maafisa wa ngazi ya chini.

Baadhi ya watu waliopatikana na virusi ni wale waliotangamana kwa karibu na Bw. Trump walipohudhuria mkutano ndani ya White House mwezi Septemba tarehe 26. Mkutano huo unasadikiwa kuwa chimbuko la “mlipuko wa virusi” .

Ikulu ya White House haijatoa orodha kamili inayoonesha ni wafanyakazi wangapi wamepatikana na virusi tangu Bw. Trump alipothibitishwa kuwa na corona.

Mtu wa hivi katibuni kupatikana na virusi alikuwa amehudhuria mkutano huo ambao rais alitumia kumtangaza mteuzi wake katika Mahakama ya juu zaidi nchini Marekani na kiongozi mmoja wa kidini.

Kabla ya kuhudhuria mkutano huo wa White House, Mchungaji Greg Laurie pia alikuwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence katika matembezi ya maombi katika eneo la Washington

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *