Rais Trump anaamini Saudi Arabia itarekebisha uhusiano na Israel, on September 16, 2020 at 5:00 pm

September 16, 2020

 Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini Saudi Arabia itafuata Bahrain na Falme za Kiarabu (UAE) katika kurekebisha kabisa uhusiano na Israeli.Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Saudia ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo anaamini ziko katika hatihati ya kufungua uhusiano wa kidiplomasia na Tel Aviv, akisema kwamba baada ya kuzungumza na Mfalme Salman, anafikiria nchi hiyo itafanya hivyo “kwa wakati unaofaa.””Tuna nchi nyingine nyingi ambazo zitajiunga nasi, na watajiunga nasi hivi karibuni,” Trump alisema saa chache baada ya Bahrain na UAE kutia saini rasmi hati za kurekebisha uhusiano na Israeli.”Tutakuwa na nchi 7 au 8 au 9. Tutakuwa na nchi zingine nyingi zitakazojiunga nasi, zikiwemo nchi kubwa” alisema Trump.Wakati wa hafla rasmi ya kutiwa saini Jumanne, Trump alisema makubaliano hayo yataimaliza “miongo kadhaa ya mgawanyiko na mizozo” katika eneo hilo na kuleta “mwazo wa Mashariki ya Kati mpya.””Shukrani kwa ujasiri wa viongozi wa nchi hizi tatu, tunachukua hatua kubwa kuelekea siku za usoni ambapo watu wa dini zote na asili zote wataishi pamoja kwa amani na ustawi,” Trump alisema, akihutubia mamia ya wageni waliokusanyika katika hafla hiyo Ikulu.Bahrain imekuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli Ijumaa iliyopita baada ya Misri mnamo 1979, Jordan mnamo 1994 na UAE mnamo mwezi Agosti.Mbali na makubaliano ya nchi mbili yaliyosainiwa kati ya Israeli na mataifa ya Kiarabu, nchi hizo tatu zimetia saini makubaliano ya “Abraham Accords” na nchi ya Marekani.Waziri wa Mambo ya nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Alzayani ameelezea makubaliano hayo kama “hatua muhimu ya kwanza” kuelekea kuanzisha amani zaidi katika eneo hilo.”Sasa ni jukumu letu kufanya kazi haraka na kwa bidii kuleta amani na usalama wa kudumu ambao watu wetu wanastahili. Suluhisho la haki, pana na la kudumu la serikali mbili kwa mzozo wa Palestina na Israeli litakuwa msingi wa amani” alisema Alzayani.Makubaliano hayo yameshambuliwa na Palestina na kwamba hayana faida yoyote kwa taifa hilo na yanapuuza haki zao.Mamlaka ya Palestina yameisema makubaliano yoyote na Israeli yanapaswa kutegemea Mpango wa Amani wa Kiarabu wa 2002 juu ya kanuni ya “ardhi kwa amani” na sio “amani kwa amani” kama Israeli inavyodumisha.,

 

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini Saudi Arabia itafuata Bahrain na Falme za Kiarabu (UAE) katika kurekebisha kabisa uhusiano na Israeli.

Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Saudia ni miongoni mwa nchi kadhaa ambazo anaamini ziko katika hatihati ya kufungua uhusiano wa kidiplomasia na Tel Aviv, akisema kwamba baada ya kuzungumza na Mfalme Salman, anafikiria nchi hiyo itafanya hivyo “kwa wakati unaofaa.”

“Tuna nchi nyingine nyingi ambazo zitajiunga nasi, na watajiunga nasi hivi karibuni,” Trump alisema saa chache baada ya Bahrain na UAE kutia saini rasmi hati za kurekebisha uhusiano na Israeli.

“Tutakuwa na nchi 7 au 8 au 9. Tutakuwa na nchi zingine nyingi zitakazojiunga nasi, zikiwemo nchi kubwa” alisema Trump.

Wakati wa hafla rasmi ya kutiwa saini Jumanne, Trump alisema makubaliano hayo yataimaliza “miongo kadhaa ya mgawanyiko na mizozo” katika eneo hilo na kuleta “mwazo wa Mashariki ya Kati mpya.”

“Shukrani kwa ujasiri wa viongozi wa nchi hizi tatu, tunachukua hatua kubwa kuelekea siku za usoni ambapo watu wa dini zote na asili zote wataishi pamoja kwa amani na ustawi,” Trump alisema, akihutubia mamia ya wageni waliokusanyika katika hafla hiyo Ikulu.

Bahrain imekuwa nchi ya nne ya Kiarabu kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli Ijumaa iliyopita baada ya Misri mnamo 1979, Jordan mnamo 1994 na UAE mnamo mwezi Agosti.

Mbali na makubaliano ya nchi mbili yaliyosainiwa kati ya Israeli na mataifa ya Kiarabu, nchi hizo tatu zimetia saini makubaliano ya “Abraham Accords” na nchi ya Marekani.

Waziri wa Mambo ya nje wa Bahrain Abdullatif bin Rashid Alzayani ameelezea makubaliano hayo kama “hatua muhimu ya kwanza” kuelekea kuanzisha amani zaidi katika eneo hilo.

“Sasa ni jukumu letu kufanya kazi haraka na kwa bidii kuleta amani na usalama wa kudumu ambao watu wetu wanastahili. Suluhisho la haki, pana na la kudumu la serikali mbili kwa mzozo wa Palestina na Israeli litakuwa msingi wa amani” alisema Alzayani.

Makubaliano hayo yameshambuliwa na Palestina na kwamba hayana faida yoyote kwa taifa hilo na yanapuuza haki zao.

Mamlaka ya Palestina yameisema makubaliano yoyote na Israeli yanapaswa kutegemea Mpango wa Amani wa Kiarabu wa 2002 juu ya kanuni ya “ardhi kwa amani” na sio “amani kwa amani” kama Israeli inavyodumisha.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *