Rais Samia ateua bosi mpya Tanroads

July 30, 2021

 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Rogatus Mativila kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads).

Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Julai 30, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema kuwa Mativila ameteuliwa kuchukua nafasi ya marehemu Mhandisi Patrick Mfugale ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021.

Kabla ya uteuzi huo Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

Pia, taarifa hiyo imesema kuwa, mkuu huyo wa nchi amemteua Profesa Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (Tafico).

Kabla ya uteuzi huo Profesa Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.

 Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Julai 28, 2021.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *