Rais Magufuli awataka walimu kulipuuza tangazo la kufutwa kwa mtaala wa ualimu ngazi ya cheti

October 5, 2020

Katika kusherehekea Siku ya Walimu duniani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Magufuli amewatoa hofu walimu huku akiwataka walimu kulipuuza tangazo lililopo katika mitandao linalohusu kufutwa kwa mtaala wa ualimu ngazi ya cheti.

Akizungumza moja kwa moja kwa njia ya simu katika Kongamano la Maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani Rais Magufuli amesema kuwa serikali inawathamini walimu huku wote wakiwemo walimu wa cheti na kwamba serikali imetangaza nafasi elfu 13 ili kuwapunguzia mzigo mkubwa walionao walimu ambapo yeye binafsi anatambua machungu ya walimu.

Akimuwakilisha Waziri Mkuu katika Kongamano hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe Jenista Mhagama amesema kuwa walimu ni watu muhimu sana katika jamii huku akiwataka viongozi serikali katika ngazi mbalimbali kushughulikia maswala ya walimu kwa kuongozwa na uzalendo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *