Rais hawezi kuingilia hali ya hewa- Rais wa Senegal, on September 18, 2020 at 6:00 am

September 18, 2020

 Macky Sall ametembelea kitongoji cha Keur Massar, kilomita 20 kutoka Dakar, mji mkuu, ambao ulikumbwa na janga la mafuriko kote nchini mnamo 5-6 Septemba.Sall, ambaye amefanya uchunguzi katika mkoa huo, amepinga ukosoaji wa miundombinu na kutumia maneno yafuatayo,”Mvua zilikuwa kubwa sana, lakini rais hawezi kuzuia matukio ya hali ya hewa.”Sall pia ameutaka umma usijenge nyumba katika maeneo yenye kunyesha mvua kubwa.Mnamo Septemba 5, nchi hiyo ilipigwa na mvua kubwa kuliko wastani wa kipindi cha mvua cha miezi 3 (Julai-Septemba).Watu 7 walifariki katika janga hilo, na watu 16,798 wameathiriwa na mafuriko.Msimu wa mvua katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ulianza mnamo Juni, unaendelea hadi Septemba.Mvua kubwa pia imesababisha mafuriko huko Niger na Burkina Faso mwaka huu.Watu wasiopungua 65 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Niger tangu mwanzoni mwa Juni.,

 

Macky Sall ametembelea kitongoji cha Keur Massar, kilomita 20 kutoka Dakar, mji mkuu, ambao ulikumbwa na janga la mafuriko kote nchini mnamo 5-6 Septemba.

Sall, ambaye amefanya uchunguzi katika mkoa huo, amepinga ukosoaji wa miundombinu na kutumia maneno yafuatayo,

“Mvua zilikuwa kubwa sana, lakini rais hawezi kuzuia matukio ya hali ya hewa.”

Sall pia ameutaka umma usijenge nyumba katika maeneo yenye kunyesha mvua kubwa.

Mnamo Septemba 5, nchi hiyo ilipigwa na mvua kubwa kuliko wastani wa kipindi cha mvua cha miezi 3 (Julai-Septemba).

Watu 7 walifariki katika janga hilo, na watu 16,798 wameathiriwa na mafuriko.

Msimu wa mvua katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, ulianza mnamo Juni, unaendelea hadi Septemba.

Mvua kubwa pia imesababisha mafuriko huko Niger na Burkina Faso mwaka huu.

Watu wasiopungua 65 wamepoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Niger tangu mwanzoni mwa Juni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *