Rais Hassan Rouhani: Iran “itajibu vikali uonevu wa Marekani”

September 21, 2020

Dakika 2 zilizopita

Uchumi wa Iran uliathirika kufuatia vikwazo ulivyowekewa

Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani “imeshindwa” katika juhudi zake za kuiwekea tena vikwazo nchi hiyo baada ya washirika wake wa Ulaya kusema hatua hiyo haiambatani na msingi wa kisheria.

Katika hotuba iliyopeperushwa kupitia televisheni, Bwana Rouhani alisema Iran “itajibu vikali uonevu wa Marekani”.

Utawala wa Marekani umesema vikwazo hivyo vinarejelewa tena chini ya mkataba wa nyuklia ambao Marekani ilijiondoa .

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimesema hazina uwezo wa kutekeleza hatua kama hiyo .

Nchi hizo tatu – pamoja na China, Urusi na Marekani – zilitia saini mkataba 2015 kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran.

Lakini Rais Donald Trump, mkosoaji wa mkataba huo ulioafikiwa wakati wa utawala wa Obama, aliiondoa Marekani 2018.

Kutokana na hilo, Iran ilianza kukiuka baadhi ya ahadi ilizotoa ikiwa ni pamoja na urutubishaji wa madini ya uranium zaidi ya kiwango kilichowekwa.

Marekani ilisema nchi hiyo inastahili kuchukuliwa hatua, na kutangaza kuwa vikwazo vyote vya Umoja wa Mataifa ambavyo vilikuwa vimesitishwa virudishwe tena – hatua ambayo ilikuwa “imegonga mwamba” – na kwamba vikwazo vya silaha dhidi ya Iran havitaisha Oktoba 18.

Lakini tangazo la Washington’limepuuziliwa mbali na Carib kilt mwanachama wa Baraza la Umoja wa Kimataifa, na haikuendeleza hatua hiyo tena. Athari za uamuzi huo haijajulikani .

Siku ya Jumamosi, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa aliiambia shirika la habari la Reuters kwamba kuanzia Jumatatu, Washington huenda ikaanza kuwawekea vikwazo baadhi ya watu na mashirika yatakayojihusisha na zana za nyukilia za Iran, makombora na mpango wake wa uundaji silaha ndogo ndogo

Iran inasema nini?

Katika hotuba yake, Bwana Rouhani aliongeza kuwa: “Marekani imeanza kushindwa katika hatua yake… Ilikabiliwa na changamoto na jibu hasi kutoka kwa jamii ya kimataifa.”

Rais Trump na Hassan Rouhani

Awali, wizara ya mambo ya kigeni ya Iran, ilitaja hatua ya Marekani kuwa “bure”, ikisema kuwa “vitendo vya Marekani ni tisho kubwa kwa usalama wa kimataifa na tisho ambalo halijawahi kukumba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa”.

“Iran inasisitiza kwamba ikiwa Marekani, moja kwa moja ama kwa ushirikiano na washirika wake, watachukua hatua yoyote kutokana na vikwazo hivi, watakabiliwa vikali na watawajibikia hatua hiyo,” ilisema katika taarifa yake, bila kufafanua.

Hatua hiyo imepokelewaje kimataifa?

Uingereza,Ufaransa na Ujerumani ambao ni wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, zinasema tangazo la Washington “

haliwezi kuwa na athari yoyote ya kisheria

” kwa sababu Marekani imetumia mfumo wa mkataba ambao haitekelezi tena.

”Tunafanya kazi kwa bidiii kudumisha mkataba wa nyuklia na tumejitolea kufanya hivyo.”

Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi ambaye ni mwanachama mwengine wa kudumu katika Baraza la Usalama, ilisema: “Mpango huo unakiuka sheria na hivyo basi hatua ya Marekani haiwezi kuwa na athari zozote za sheria kimataifa kwa nchi zingine.”

Siku ya Jumamosi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alilifahamisha Baraza la Usalama la Umoja huo kwamba hana uwezo wa kuchukua hatua yoyote kwa sababu ya “sintofahamu inayokumba” suala hilo. Lakini maafisa wa Marekani wanasema, licha ya kwamba nchi hiyo ilijiondoa katika mkataba wa nyuklia, bado ina haki ya “kutekeleza” tena kifungu cha sheria.

Tangazo hilo liltolewa siku 30 baada ya Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kulifahamisha baraza hilo kwamba utawala huo unatekeleza vikwazo hivyo.

Katika taarifa situ ya Jumamosi, bwana Pompeo alisema hatua itatangazwa siku chache zijazo dhidi ya chi ambazo hazitatekeleza vikwazo bila kutoa maelezo.

Baada ya kujiondoa Katika mkataba huo Marekani ilifufua tena vikwazo dhidi ya Iran, hali ambayo imelemeza uchumi wa nchi hiyo ambayo pia imeathiriwa vibaya na jana la Covid-19.

Tangazo hilo linakuja karibu wiki sita kabla ya uchaguzi mkuu wa urais Marekani. Bwana Trump atakabiliana na mpinzani wake wa Democratic Joe Biden ambaye ameahidi kurudisha Marekani katika makubaliano hayo.

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, ATTA KENARE VIA GETTY Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema Marekani “imeshindwa” katika juhudi…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *