Rais Erdogan azidisha cheche za maneno kwenye mvutano na Ugiriki, on September 6, 2020 at 7:00 am

September 6, 2020

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, ameionya Ugiriki kuingia katika mazungumzo kuhusu eneo linalozozaniwa la mashariki mwa bahari Mediterrania, au waathiriwe.Akizungumza katika hafla ya kufungua hospitali mjini Istanbul, Erdogan amesema, Ugiriki italazimika kuelewa lugha ya siasa na diplomasia au uwanjani kwa madhara machungu.Uturuki inazozana na Ugiriki pamoja na Cyprus kuhusu haki za kutafuta gesi na mafuta mashaeriki mwa bahari Mediterrania.Pande zote kwenye mvutano huo zimepeleka vikosi vya jeshi vya majini na angani kutetea madai yao katika eneo hilo.Hayo yakijiri, gazeti la Cumhuriyet la Uturuki limeripoti kuwa vifaru 40 vya kijeshi vimekuwa vikisafirishwa kutoka mpaka wa Syria kuelekea Edirne, kaskazini magharibi mwa Uturuki.,

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan, ameionya Ugiriki kuingia katika mazungumzo kuhusu eneo linalozozaniwa la mashariki mwa bahari Mediterrania, au waathiriwe.

Akizungumza katika hafla ya kufungua hospitali mjini Istanbul, Erdogan amesema, Ugiriki italazimika kuelewa lugha ya siasa na diplomasia au uwanjani kwa madhara machungu.

Uturuki inazozana na Ugiriki pamoja na Cyprus kuhusu haki za kutafuta gesi na mafuta mashaeriki mwa bahari Mediterrania.

Pande zote kwenye mvutano huo zimepeleka vikosi vya jeshi vya majini na angani kutetea madai yao katika eneo hilo.

Hayo yakijiri, gazeti la Cumhuriyet la Uturuki limeripoti kuwa vifaru 40 vya kijeshi vimekuwa vikisafirishwa kutoka mpaka wa Syria kuelekea Edirne, kaskazini magharibi mwa Uturuki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *