Rais Edroğan: Hatuwezi kuvumilia unyanyasaji wa wanawake,

October 2, 2020

Rais Erdoğan alihudhuria mkutano wa 4 wa kuadhimisha miaka 25 ya kongamano la wanawake ulioandaliwa chini ya usimamizi wa baraza kuu la 75 la Umoja wa Mataifa.

Rais Erdoğan alishiriki mkutano huo kwa njia ya mawasiliano ya video.

Katika maelezo yake, Erdoğan aliongezea kusema,

“Sisi kama Uturuki tumeweza kuchukua hatua kama ilivyokuwa sifa yetu ya kihistoria kuimarisha hadhi ya wanawake na majukumu ya maisha ya kijamii katika miaka ya hivi karibuni. Kwa kuzingatia kanuni ya ‘Nguvu kwa mwanamke, nguvu kwa familia, nguvu kwa jamii’, tumehimiza elimu na ushirikisho wa nguvukazi kwa wanawake na mabinti wa kike kwa ujumla.’’

Akigusia suala la mapambano dhidi ya unyanyasaji wa wanawake, Erdoğan aliongezea kusema, ‘‘Tunaendeleza harakati za kutetea haki za wanawake na kukabiliana na suala la unyanyasahi dhidi yao. Hatuwezi kuvumilia ukiukaji wa haki, sheria wala utu dhidi ya mwanamke hata mmoja katika nchi yetu.’’

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *