Rais aliyepinduliwa wa Mali apelekwa nje ya nchi kwa matibabu

September 6, 2020

Rais aliyepinduliwa wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kutibiwa. Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na mke wake, madaktari wawili, mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi. Tangu Keita mwenye umri wa miaka 75 alipolazwa hospitalini, baada ya kuwekwa kizuizini kwa siku 10 na wanajeshi waliompindua, maswali mengi yameulizwa kuhusu hali yake ya afya. Katika tukio jingine, mazungumzo kuhusu utakaokuwa utawala wa mpito nchini Mali yameanza jana Jumamosi mjini Bamako. Mamia ya wawakilishi wa vyama vya kisiasa pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu walihudhuria ufunguzi wa mazungumzo hayo.,

Rais aliyepinduliwa wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, amesafirishwa kupelekwa Umoja wa Falme za Kiarabu kutibiwa. 

Mwanadiplomasia mmoja ambaye hakutaka kutambulishwa jina lakini anafahamu tukio hilo, amesema hayo na kuongeza kwamba Keita ameondoka akiwa pamoja na mke wake, madaktari wawili, mawakala wanne wa kiusalama na msaidizi. 

Tangu Keita mwenye umri wa miaka 75 alipolazwa hospitalini, baada ya kuwekwa kizuizini kwa siku 10 na wanajeshi waliompindua, maswali mengi yameulizwa kuhusu hali yake ya afya. 

Katika tukio jingine, mazungumzo kuhusu utakaokuwa utawala wa mpito nchini Mali yameanza jana Jumamosi mjini Bamako. Mamia ya wawakilishi wa vyama vya kisiasa pamoja na makundi ya kutetea haki za binadamu walihudhuria ufunguzi wa mazungumzo hayo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *