R Kelly Akutana na Kisanga Kingine Gerezani, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 3, 2020

STAA wa muziki wa kiwango cha Dunia kutoka nchini Marekani, Robert Kelly ‘R Kelly’, amekutana na kisanga cha kushambuliwa na mahabusu mwenzake gerezani, ambako anasubiri hukumu ya kesi yake.Akizungumzia ishu hiyo, mwanasheria wa R Kelly, Steve Greenberg amesema, mteja wake huyo alishambuliwa katika gereza hilo la Chicago Metropolitan Collection Center, ambako R Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya unyanyasaji wa kingono wa wanawake.Mahabusu mwenzake na R Kelly, alimshambulia alipokuwa amekaa kwenye kitanda kwa kumpiga ngumi sababu ikiwa kusitishwa kwa kutembelewa gerezani kutokana na mashabiki wa R Kelly wanaoandamana nje ya gereza hilo.R Kelly amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushindwa kupewa dhamana ambapo kesi yake hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Septemba.,

STAA wa muziki wa kiwango cha Dunia kutoka nchini Marekani, Robert Kelly ‘R Kelly’, amekutana na kisanga cha kushambuliwa na mahabusu mwenzake gerezani, ambako anasubiri hukumu ya kesi yake.

Akizungumzia ishu hiyo, mwanasheria wa R Kelly, Steve Greenberg amesema, mteja wake huyo alishambuliwa katika gereza hilo la Chicago Metropolitan Collection Center, ambako R Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake ya unyanyasaji wa kingono wa wanawake.

Mahabusu mwenzake na R Kelly, alimshambulia alipokuwa amekaa kwenye kitanda kwa kumpiga ngumi sababu ikiwa kusitishwa kwa kutembelewa gerezani kutokana na mashabiki wa R Kelly wanaoandamana nje ya gereza hilo.

R Kelly amekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushindwa kupewa dhamana ambapo kesi yake hiyo, inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwezi Septemba.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *