Queen Darleen na Mke Mwenza Gari Limewaka

September 18, 2020

MSANIIwa Bongo Fleva ambaye kwa sasa ni mke wa pili wa Isihaka Mtoro, mwanadada ‘Queen Darleen’ ameanza kuvaana na mke mwenziye anayefahamika kwa jina la Sabra kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.Hayo yamejiri baada ya wawili hao; Queen Darleen na Sabra kuanza kutupiana madongo kwenye mitandao ya kijamii, huku kila mmoja akitamba kupendwa.Mke mdogo ambaye ni Queen Darleen, alianza kwa kutuma video fupi iliyoonekana akikumbatia picha ya mume wao Isihaka, jambo lililoleta wivu na kupelekea mke mkubwa (Sabra) kuingia hewani (live) na kumrekodi kwa mbali mume wao Isihaka akiwa kitandani huku akiwa tumbo waziBaada ya muda kidogo, Queen Darleen aliandika ujumbe mfupi wa kejeli akimjibu mke mkubwa akisema “Naskia kuna mtu kaingia Insta live kwake, lakini anashut kama jambazi kaingia nyumbani na kuiba Sh milioni 10 na mjegejoo, baba ovyooo.”Hatua hiyo, ilisababisha Sabra kujibu na kuandika ujumbe, “Hivi na nyie mnapendwa kama mimi…? huba linanizidia natamani kutoa ushuhuda mwenzenu… napendwa alafu napendwa tena,” alisema Sabra.Majibizano haya ya mitandaoni ya wake wenza hao ambayo yameonekana kuwa sawa na kutupa jiwe gizani, yamezua sintofahamu kwa mashabiki zao.Mmoja wa mashabiki waliandika katika ukurasa huo kumponda Queen Darleen na kumuonya kuwa aache kidomodomo,

MSANIIwa Bongo Fleva ambaye kwa sasa ni mke wa pili wa Isihaka Mtoro, mwanadada ‘Queen Darleen’ ameanza kuvaana na mke mwenziye anayefahamika kwa jina la Sabra kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Hayo yamejiri baada ya wawili hao; Queen Darleen na Sabra kuanza kutupiana madongo kwenye mitandao ya kijamii, huku kila mmoja akitamba kupendwa.

Mke mdogo ambaye ni Queen Darleen, alianza kwa kutuma video fupi iliyoonekana akikumbatia picha ya mume wao Isihaka, jambo lililoleta wivu na kupelekea mke mkubwa (Sabra) kuingia hewani (live) na kumrekodi kwa mbali mume wao Isihaka akiwa kitandani huku akiwa tumbo wazi

Baada ya muda kidogo, Queen Darleen aliandika ujumbe mfupi wa kejeli akimjibu mke mkubwa akisema “Naskia kuna mtu kaingia Insta live kwake, lakini anashut kama jambazi kaingia nyumbani na kuiba Sh milioni 10 na mjegejoo, baba ovyooo.

”Hatua hiyo, ilisababisha Sabra kujibu na kuandika ujumbe, “Hivi na nyie mnapendwa kama mimi…? huba linanizidia natamani kutoa ushuhuda mwenzenu… napendwa alafu napendwa tena,” alisema Sabra.

Majibizano haya ya mitandaoni ya wake wenza hao ambayo yameonekana kuwa sawa na kutupa jiwe gizani, yamezua sintofahamu kwa mashabiki zao.Mmoja wa mashabiki waliandika katika ukurasa huo kumponda Queen Darleen na kumuonya kuwa aache kidomodomo

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *