Queen Darleen Aongelea Bifu lake na Dada yake Esma Platnumz

September 15, 2020

Baada ya kuwepo kwa madai mazito kwamba, wapo kwenye bifu zito, hatimaye dada wa mwanamuziki mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amevunja ukimya. Darleen amefunguka juu ya kuwepo kwa bifu kali kati yake na ndugu yake, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.Awali, wananzengo walianza kusambaza habari za warembo hao kuwa na bifu kali, baada ya Esma ambaye naye ni dada wa Diamond au Mondi, kutoonekana kwenye shughuli ya baby shower ya ndugu yake, Darleen iliyofanyika nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar, wikiendi iliyopita.“Unaambiwa Esma na Queen (Darleen) wana bifu la muda mrefu sana, lakini wakiwa kwenye mikusanyiko, ndipo huwa wanajifanya wanaongea. “Inasemekana chanzo cha bifu lao ni madai ya mume wa Esma, Yahaya Msizwa, kwamba eti amewahi kuwa ‘sponsa’ wa Queen (Darleen),” kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kuhifadhiwa jina gazetini.Baada ya tetesi hizo kuzidi kusambaa kama moto wa kifuu, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limemtafuta Queen Darleen ili kufahamu ukweli wa jambo hilo, na kama tayari amejifungua au bado.IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Queen Darleen?QUEEN DARLEEN: Poa, niambie…IJUMAA WIKIENDA: Safi tu, kuna tetesi kuwa umeshajifungua ila hutaki kuweka wazi na inasemekana hata ile baby shower ilifanyika muda mrefu, ila picha ndiyo mmeanza kuzivujisha juzi, hili lina ukweli kiasi gani?QUEEN DARLEEN: Hapana, bado sijajifungua, ile baby shower ilifanyika juzi tu pale nyumbani kwangu (MbeziBeach), nikishajifungua kila mtu atajua.IJUMAA WIKIENDA: Pia inasemekana kwamba, Esma hakufika kwenye baby shower yako kwa sababu ya bifu lenu kubwa mlilonalo, hili likoje?QUEEN DARLEEN: Unajua kuna kitu watu hawakijui, ile baby shower mimi nilifanyiwa na rafiki zangu, siyo familia yangu. Ndiyo maana Esma hakuonekana, Mama Dangote (Mama Diamond), Nasibu (Mondi) na ndugu zangu wengine wa karibu, nao hawakuwepo.Sasa kwa nini watu wamseme Esma peke yake ndiye hakuja wakati kuna ndugu zangu wengine wengi tu, nao hawakuja? Ina maana mimi nina ndugu watatu tu? Watu waache kuongea mambo ambayo hawana uhakika nayo, mimi sina bifu na Esma, ni ndugu yangu na nampenda, mengine watuachie wenyewe.IJUMAA WIKIENDA: Asante sana, nakutakia kila la heri.QUEEN DARLEEN: Inshaallah, nashukuru sana.UFAFANUZIQueen Darleen na Esma, kila mmoja ana baba yake. Queen Darleen baba yake ni Mzee Abdul Juma (Baba D) wakati Esma baba yake ni Mzee Khan. Queen Darleen na Esma ni ndugu, kwani wote ni damu moja na Mondi ambapo kwa upande wa mama (Esma) au kwa upande wa baba (Queen Darleen).,

Baada ya kuwepo kwa madai mazito kwamba, wapo kwenye bifu zito, hatimaye dada wa mwanamuziki mkubwa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amevunja ukimya. Darleen amefunguka juu ya kuwepo kwa bifu kali kati yake na ndugu yake, Esma Khan ‘Esma Platnumz’.

Awali, wananzengo walianza kusambaza habari za warembo hao kuwa na bifu kali, baada ya Esma ambaye naye ni dada wa Diamond au Mondi, kutoonekana kwenye shughuli ya baby shower ya ndugu yake, Darleen iliyofanyika nyumbani kwake, Mbezi-Beach jijini Dar, wikiendi iliyopita.

“Unaambiwa Esma na Queen (Darleen) wana bifu la muda mrefu sana, lakini wakiwa kwenye mikusanyiko, ndipo huwa wanajifanya wanaongea. “Inasemekana chanzo cha bifu lao ni madai ya mume wa Esma, Yahaya Msizwa, kwamba eti amewahi kuwa ‘sponsa’ wa Queen (Darleen),” kilisema chanzo kimoja kwa sharti la kuhifadhiwa jina gazetini.

Baada ya tetesi hizo kuzidi kusambaa kama moto wa kifuu, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limemtafuta Queen Darleen ili kufahamu ukweli wa jambo hilo, na kama tayari amejifungua au bado.

IJUMAA WIKIENDA: Mambo vipi Queen Darleen?

QUEEN DARLEEN: Poa, niambie…

IJUMAA WIKIENDA: Safi tu, kuna tetesi kuwa umeshajifungua ila hutaki kuweka wazi na inasemekana hata ile baby shower ilifanyika muda mrefu, ila picha ndiyo mmeanza kuzivujisha juzi, hili lina ukweli kiasi gani?

QUEEN DARLEEN: Hapana, bado sijajifungua, ile baby shower ilifanyika juzi tu pale nyumbani kwangu (MbeziBeach), nikishajifungua kila mtu atajua.

IJUMAA WIKIENDA: Pia inasemekana kwamba, Esma hakufika kwenye baby shower yako kwa sababu ya bifu lenu kubwa mlilonalo, hili likoje?

QUEEN DARLEEN: Unajua kuna kitu watu hawakijui, ile baby shower mimi nilifanyiwa na rafiki zangu, siyo familia yangu. Ndiyo maana Esma hakuonekana, Mama Dangote (Mama Diamond), Nasibu (Mondi) na ndugu zangu wengine wa karibu, nao hawakuwepo.

Sasa kwa nini watu wamseme Esma peke yake ndiye hakuja wakati kuna ndugu zangu wengine wengi tu, nao hawakuja? Ina maana mimi nina ndugu watatu tu? Watu waache kuongea mambo ambayo hawana uhakika nayo, mimi sina bifu na Esma, ni ndugu yangu na nampenda, mengine watuachie wenyewe.

IJUMAA WIKIENDA: Asante sana, nakutakia kila la heri.

QUEEN DARLEEN: Inshaallah, nashukuru sana.

UFAFANUZI

Queen Darleen na Esma, kila mmoja ana baba yake. Queen Darleen baba yake ni Mzee Abdul Juma (Baba D) wakati Esma baba yake ni Mzee Khan. Queen Darleen na Esma ni ndugu, kwani wote ni damu moja na Mondi ambapo kwa upande wa mama (Esma) au kwa upande wa baba (Queen Darleen).

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *