Q Boy amuita Young Dee ni Yuda

October 4, 2020

Mbunifu wa mavazi maarufu nchini na Msanii wa kizazi kipya, Q Boy, amesema kuwa yeye siyo sababu ya Young Dee kushindwa kupendeza katika video ya Bongo bahati mbaya na kuwa alimsaidia tu baada ya kugundua alikuwa na matatizo.

Q Boy amefunguka hayo kupita eNewz ya East Africa TV kipindi kinachoruka  kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa  Saa  12:00 jioni ambapo Q Boy amesema kuwa Young Dee alipokuwa katika misukosuko aliamua kuwa upande wake na kutengeneza naye muonekano bora katika video ya bongo bahati mbaya ,ambayo ilimrudisha vyema kwenye game .

“Nilimfanyia hiyo video nikiwa na roho safi kabisa kwanza alikuwa katoka katika misukosuko mingi ila alipofanya bongo bahati mbaya, ilimrudisha lakini baadae  Young Dee akinisaliti kwa kusema kuwa sijawahi kumvalisha poa sawa tu hata Yesu alisalitiwa na Yuda na bado maisha yakaendelea.  Siwezi kumshangaa mkataba wetu uliisha ndiyo sababu sikutaka kuendelea naye kikazi “.amesema Q Boy.

 

Aidha ameongeza kuwa hadhani kama yeye ndiyo chanzo cha Young Dee kuwa na muonekano mbaya, “sidhani kama ni kweli mimi ndiyo chanzo cha Young Dee kushindwa kuonekana kung’aa katika video zake  sababu nilivyomaliza kufanya kazi na Young Dee nilirudi Afrika Kusini kwanza.Bongo bahati mbaya ndiyo video ambayo alipendeza kuliko video zake zote na hajawahi kupendeza katika video zake“, amesema Q Boy

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *