Precision Air ilitarajiwa kufanya safari kuelekea Nairobi siku ya Alhamisi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 2, 2020 at 10:00 am

September 2, 2020

Shirika la ndege Precison Air lenye makazi yake Tanzania limefuta mipango ya kuanza kwa safari za ndege kuelekea Nairobi baada ya serikali ya Kenya kusema kuwa haitafuta haki za usafiri za kampuni hiyo, wakati huu kukiwa na mvutano baina ya nchi hizo mbili, gazeti la Business Daily limeandika.Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa twitter, imesema inaahirisha mipango hiyo kwasababu ya idadi ndogo ya wateja wanaotaka kusafiri, ikiahidi kuwa tarehe nyingine ya safari kuelekea Nairobi itapangwa na kuchapishwa kwenye tovuti yao hivi karibuni.Tanzania ilizipiga marufuku kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuingia nchini humo kama hatua ya kulipiza kisasi vita vya kibiashara ambavyo vimekuwepo kati ya mataifa hayo .Hatua hiyo iliochukuliwa na Tanzania inajiri baada ya Nairobi , kwa mara ya pili mfululizo, kuiweka Tanzania miongoni mwa mataifa ambayo sio salama kutokana na virusi vya corona.Hatua hiyo ina maana kwamba wasafiri kutoka Tanzania wataendelea kukabiliwa na masharti ya lazima ya kuwekwa katika karantini kwa wiki mbili wanapowasili Kenya ili kuzuia maambukizi ya maradhi hayo.Wasafiri kutoka mataifa 130, hatahivyo wako huru kuingia nchini Kenya bila masharti yoyote kufuatia hatua ya pili ambapo serikali iliongeza mataifa mengine 90 katika orodha yake ya mataifa yanayostahili kuingia nchini humo.Mvutano huu umeathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili. Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Airways Allan Kilavuka alisema kwamba njia ya kuelekea Tanzania inasalia kuwa muhimu kutokana na idadi ya wateja inaowaleta Kenya kwa safari nyingine za kimataifa kwa kutumia ndege za kampuni hiyo.Tunatumai kwamba tatizo hili litatatuliwa haraka iwezekanavyo , alisema bwana Kilavuka.Precision Air itarajiwa kuanza safari kutoka Dar es Salaam kupitia Zanzibar kuelekea Nairobi na kurudi.Katika hatua nyingine, wadau wa sekta ya utalii wametahadharisha kuhusu mvutano katika sekta ya usafiri wa anga kati ya Kenya na Tanzania kuhusu vikwazo vya kusafiri hali ambayo wameeleza kuwa italeta athari katika sekta hiyo.Wadau hao wameitaka Kenya kufikiria tena msimamo wake kuhusu wasafiri Watanzania, ambao wanapaswa kukaa karantini kwa siku 14 wanapoingia jijini Nairobi.Wadau wa sekta ya utalii wakiongozwa Mohammed Hersi wa Shirikisho la taasisi zinazoshughulika na masuala ya utalii Kenya (KTF) amenukuliwa na Business Daily akisema kuwa namna ambavyo Kenya inawatendea Tanzania kutaathiri sekta ya usafiri wa anga.Mzozo wa kidiplomasia utafanya jitihada za kufufua shirika la ndege la Kenya, ambalo tayari limepigwa marufuku kuingia Tanzania.,

Shirika la ndege Precison Air lenye makazi yake Tanzania limefuta mipango ya kuanza kwa safari za ndege kuelekea Nairobi baada ya serikali ya Kenya kusema kuwa haitafuta haki za usafiri za kampuni hiyo, wakati huu kukiwa na mvutano baina ya nchi hizo mbili, gazeti la Business Daily limeandika.

Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa twitter, imesema inaahirisha mipango hiyo kwasababu ya idadi ndogo ya wateja wanaotaka kusafiri, ikiahidi kuwa tarehe nyingine ya safari kuelekea Nairobi itapangwa na kuchapishwa kwenye tovuti yao hivi karibuni.

Tanzania ilizipiga marufuku kampuni tatu za ndege kutoka Kenya kuingia nchini humo kama hatua ya kulipiza kisasi vita vya kibiashara ambavyo vimekuwepo kati ya mataifa hayo .

Hatua hiyo iliochukuliwa na Tanzania inajiri baada ya Nairobi , kwa mara ya pili mfululizo, kuiweka Tanzania miongoni mwa mataifa ambayo sio salama kutokana na virusi vya corona.

Hatua hiyo ina maana kwamba wasafiri kutoka Tanzania wataendelea kukabiliwa na masharti ya lazima ya kuwekwa katika karantini kwa wiki mbili wanapowasili Kenya ili kuzuia maambukizi ya maradhi hayo.

Wasafiri kutoka mataifa 130, hatahivyo wako huru kuingia nchini Kenya bila masharti yoyote kufuatia hatua ya pili ambapo serikali iliongeza mataifa mengine 90 katika orodha yake ya mataifa yanayostahili kuingia nchini humo.

Mvutano huu umeathiri biashara kati ya mataifa hayo mawili. Afisa mkuu mtendaji wa shirika la ndege la Kenya Airways Allan Kilavuka alisema kwamba njia ya kuelekea Tanzania inasalia kuwa muhimu kutokana na idadi ya wateja inaowaleta Kenya kwa safari nyingine za kimataifa kwa kutumia ndege za kampuni hiyo.

Tunatumai kwamba tatizo hili litatatuliwa haraka iwezekanavyo , alisema bwana Kilavuka.

Precision Air itarajiwa kuanza safari kutoka Dar es Salaam kupitia Zanzibar kuelekea Nairobi na kurudi.

Katika hatua nyingine, wadau wa sekta ya utalii wametahadharisha kuhusu mvutano katika sekta ya usafiri wa anga kati ya Kenya na Tanzania kuhusu vikwazo vya kusafiri hali ambayo wameeleza kuwa italeta athari katika sekta hiyo.

Wadau hao wameitaka Kenya kufikiria tena msimamo wake kuhusu wasafiri Watanzania, ambao wanapaswa kukaa karantini kwa siku 14 wanapoingia jijini Nairobi.

Wadau wa sekta ya utalii wakiongozwa Mohammed Hersi wa Shirikisho la taasisi zinazoshughulika na masuala ya utalii Kenya (KTF) amenukuliwa na Business Daily akisema kuwa namna ambavyo Kenya inawatendea Tanzania kutaathiri sekta ya usafiri wa anga.

Mzozo wa kidiplomasia utafanya jitihada za kufufua shirika la ndege la Kenya, ambalo tayari limepigwa marufuku kuingia Tanzania.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *