Poul Makonda apata watoto mapacha “katikati ya machozi umenipatia zawadi tena”, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on August 31, 2020 at 10:00 am

August 31, 2020

Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda amebahatika kwa mara nyingine watoto ambao ni mapacha wa kiumbve. Taarifa hiyo imethibitisha kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika hivi;Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakua hujawahi kuniacha hata dakika moja.Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika.Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako.Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake:Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu.Kwa wale ambao bado hawajakuamini na wanateseka juu ya uzazi,naomba kupitia watoto hawa wakauone ukuu wako Ewe YESU mwana wa Mungu ulie hai.Hongera sana kipenzi changu Maria Mungu amejitwalia utukufu kupitia wewe.Asanteni sana watumishi wa Mungu, wazazi wetu, dada na kaka zetu kwa kuwa nasi nyakati zote, kama ambavyo mmekuwa baraka kwetu.Naomba pia Mungu awainulie watu wema nyakati za uhitaji wenu.,

Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda amebahatika kwa mara nyingine watoto ambao ni mapacha wa kiumbve.

 Taarifa hiyo imethibitisha kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika hivi;

Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakua hujawahi kuniacha hata dakika moja.

Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika.

Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako.

Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake:Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu.

Kwa wale ambao bado hawajakuamini na wanateseka juu ya uzazi,naomba kupitia watoto hawa wakauone ukuu wako Ewe YESU mwana wa Mungu ulie hai.

Hongera sana kipenzi changu Maria Mungu amejitwalia utukufu kupitia wewe.

Asanteni sana watumishi wa Mungu, wazazi wetu, dada na kaka zetu kwa kuwa nasi nyakati zote, kama ambavyo mmekuwa baraka kwetu.Naomba pia Mungu awainulie watu wema nyakati za uhitaji wenu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *