Pompeo aonya kuhusu mazungumzo yanayosubiriwa ya Waafghanistan, on September 11, 2020 at 1:00 pm

September 11, 2020

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo ameonya kuwa mazungumzo yanayosubiriwa kwa hamu kati ya pande zinazohasimiana nchini Afghanistan yanatazamiwa kuwa yenye utata, lakini ndiyo njia pekee ya kusonga mbele kama Waafghanistan wanataka kupata amani baada ya miongo mingi ya mgogoro usiokuwa na mwisho. Pompeo ameyasema hayo wakati akiwa safarini kwenda katika taifa la Qatar la Mashariki ya Kati, ambako mazungumzo ya Waafghanistan yanatarajiwa kuanza kesho Jumamosi. Mazungumzo hayo yaliyokubaliwa katika mpango wa amani uliosimamiwa na Marekani na Taliban na kusainiwa Doha mnamo Februari 29 yanalenga kumaliza vita vya Afghanistan na kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.,

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo ameonya kuwa mazungumzo yanayosubiriwa kwa hamu kati ya pande zinazohasimiana nchini Afghanistan yanatazamiwa kuwa yenye utata, lakini ndiyo njia pekee ya kusonga mbele kama Waafghanistan wanataka kupata amani baada ya miongo mingi ya mgogoro usiokuwa na mwisho.

 Pompeo ameyasema hayo wakati akiwa safarini kwenda katika taifa la Qatar la Mashariki ya Kati, ambako mazungumzo ya Waafghanistan yanatarajiwa kuanza kesho Jumamosi.

 Mazungumzo hayo yaliyokubaliwa katika mpango wa amani uliosimamiwa na Marekani na Taliban na kusainiwa Doha mnamo Februari 29 yanalenga kumaliza vita vya Afghanistan na kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *