Pompeo ahimiza kuhusu suluhisho la kidiplomasia katika mvutano wa Ugiriki na Uturuki, on September 13, 2020 at 10:00 am

September 13, 2020

 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo jana ametoa wito wa suluhisho la kidiplomasia katika mzozo kati ya Uturuki na Ugiriki kuhusu maliasili ya gesi na mafuta katika eneo la mashariki mwa Mediterania na kusema mvutano wa kijeshi unaoendelea kati ya mataifa hayo mawili washirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO unawanufaisha tu mahasimu wa jumuiya hiyo. Akiwa ziarani Cyprus na baada ya mazungumzo na rais wa nchi hiyo Nicos Anastasiades, Pompeo alisema kuwa mvutano huo wa kijeshi unawanufaisha mahasimu wa NATO ambao wangetaka kuona mgawanyiko katika umoja wa mataifa ya pande zote za bahari ya Atlantiki.Pompeo amesema kuwa tayari rais Donald Trump amezungumza na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika matumaini ya kumaliza mkwamo uliopo.,

 

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo jana ametoa wito wa suluhisho la kidiplomasia katika mzozo kati ya Uturuki na Ugiriki kuhusu maliasili ya gesi na mafuta katika eneo la mashariki mwa Mediterania na kusema mvutano wa kijeshi unaoendelea kati ya mataifa hayo mawili washirika wa jumuiya ya kujihami ya NATO unawanufaisha tu mahasimu wa jumuiya hiyo. 

Akiwa ziarani Cyprus na baada ya mazungumzo na rais wa nchi hiyo Nicos Anastasiades, Pompeo alisema kuwa mvutano huo wa kijeshi unawanufaisha mahasimu wa NATO ambao wangetaka kuona mgawanyiko katika umoja wa mataifa ya pande zote za bahari ya Atlantiki.

Pompeo amesema kuwa tayari rais Donald Trump amezungumza na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis katika matumaini ya kumaliza mkwamo uliopo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *