Polisi ya Urusi inataka kumuuliza Navalny maswali nchini Ujerumani, on September 11, 2020 at 1:00 pm

September 11, 2020

Polisi ya Urusi imesema leo kuwa inapanga kumuhoji kiongozi wa upinzani Alexei Navalny mjini Berlin, baada ya serikali ya Moscow kupuuzilia mbali kauli ya Ujerumani kuwa alipewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok. Polisi ya Urusi imesema kufuatia ripoti kuwa Navalny ameanza kupata fahamu, huenda watahitaji kumuuliza maswali ya ufafanuzi na ya ziada, na wawepo wakati wenzao wa Ujerumani wakiendelea na uchunguzi wao na Navalny, madaktari na watalaamu. Serikali ya Urusi inapinga majaribio yoyote ya kuilaumu Urusi kwa tukio hilo la sumu, na inasema inataka kujua nini kilitokea. Wanasiasa wa kimataifa wanasema tukio hilo linalonekana kuamrishwa na serikali na kuitaka Urusi ithibitishe kutohusika kwake. Mkosoaji huyo wa serikali ya Urusi mwenye umri wa miaka 44 na mwanarakati wa kupambana na rushwa aliugua baada ya kupanda ndege katika mkoa wa Siberia na akalazwa huko kabla ya kusafirishwa Ujerumani.,

Polisi ya Urusi imesema leo kuwa inapanga kumuhoji kiongozi wa upinzani Alexei Navalny mjini Berlin, baada ya serikali ya Moscow kupuuzilia mbali kauli ya Ujerumani kuwa alipewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok.

 Polisi ya Urusi imesema kufuatia ripoti kuwa Navalny ameanza kupata fahamu, huenda watahitaji kumuuliza maswali ya ufafanuzi na ya ziada, na wawepo wakati wenzao wa Ujerumani wakiendelea na uchunguzi wao na Navalny, madaktari na watalaamu. 

Serikali ya Urusi inapinga majaribio yoyote ya kuilaumu Urusi kwa tukio hilo la sumu, na inasema inataka kujua nini kilitokea. 

Wanasiasa wa kimataifa wanasema tukio hilo linalonekana kuamrishwa na serikali na kuitaka Urusi ithibitishe kutohusika kwake. 

Mkosoaji huyo wa serikali ya Urusi mwenye umri wa miaka 44 na mwanarakati wa kupambana na rushwa aliugua baada ya kupanda ndege katika mkoa wa Siberia na akalazwa huko kabla ya kusafirishwa Ujerumani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *