Polisi ya Berlin yavunja maandamano dhidi ya vizuizi vya corona, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 5:00 pm

August 29, 2020

Polisi mjini Berlin leo ilivunja maandamano makubwa katika mji huo mkuu wa Ujerumani yaliyoitishwa kupinga vizuizi vya virusi vya corona saa chache tu baada ya kuanza.Hii ni baada ya waandamanaji kushindwa kuzingatia maagizo ya kutosogeleana na kuvaa maski. Maandamano hayo yamekuja wakati maambukizi yakiongezeka Ulaya na wakati hasira ya umma kuhusu hatua za kudhibiti virusi hivyo ikiongezeka katika baadhi ya maeneo. Matukio sawa na ya Berlin yalitokea Paris, London na kwingineko leo.Karibu polisi 3,000 waliwekwa katika mitaa ya Berlin kuudhibiti umati wa watu karibu 18,000. Waandamanaji walitayanyika kwa amani ijapokuwa kulikuwa na baadhi waliozusha vurugu. Polisi walikuwa wamejiandaa kwa uwezekano wa kuzuka vurugu baada ya wanaharakati wanaopinga hatua za kudhibiti virusi hivyo kuwahimiza wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii kote Ulaya kujihami na kukusanyika mjini Berlin.,

Polisi mjini Berlin leo ilivunja maandamano makubwa katika mji huo mkuu wa Ujerumani yaliyoitishwa kupinga vizuizi vya virusi vya corona saa chache tu baada ya kuanza.

Hii ni baada ya waandamanaji kushindwa kuzingatia maagizo ya kutosogeleana na kuvaa maski. Maandamano hayo yamekuja wakati maambukizi yakiongezeka Ulaya na wakati hasira ya umma kuhusu hatua za kudhibiti virusi hivyo ikiongezeka katika baadhi ya maeneo. Matukio sawa na ya Berlin yalitokea Paris, London na kwingineko leo.

Karibu polisi 3,000 waliwekwa katika mitaa ya Berlin kuudhibiti umati wa watu karibu 18,000. Waandamanaji walitayanyika kwa amani ijapokuwa kulikuwa na baadhi waliozusha vurugu. Polisi walikuwa wamejiandaa kwa uwezekano wa kuzuka vurugu baada ya wanaharakati wanaopinga hatua za kudhibiti virusi hivyo kuwahimiza wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii kote Ulaya kujihami na kukusanyika mjini Berlin.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *