Polisi wasitisha uvamizi baada ya kutokea maandamano

October 12, 2020

Dakika 9 zilizopita

endsars protest in Lagos

Maelezo ya picha,

Maandamano yameongezeka zaidi

Nigeria imevunja kikosi maalum cha polisi wakati wa maandamano dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi yanaendelea.

Serikali imesema amri rasmi kutoka kwa rais imeagiza kuvunjwa mara moja kwa kikosi maalum cha polisi cha kukabiliana na Wizi wa Mabavu (Sars).

Maandamano dhidi ya kikosi hicho yalichochewa na video ya mwanaume mmoja anaedaiwa kwamba aliuawa na polisi.

Maandamano yameongezeka licha ya kamatakamata na yamesambaa hadi nje ya Nigeria.

Je agizo la rais limesema nini?

Maafisa wote wa kikosi cha Sars – wanaoshtumiwa sana kwa ukamataji raia kinyume cha sheria, mateso na mauaji – watapelekwa kwingine, ofisi ya rais imesema na mipangilio rasmi ya kubadilisha kikosi hicho inaendelea.

Wakati huohuo, mkuu wa polisi nchini Nigeria amesema timu ya wachunguzi ikiwemo mashirika ya kiraia na haki za binadamu – yataundwa kuchunguza madai ya unyanyasaji dhidi ya kikosi hicho.

Rais Muhammadu Buhari awali alisema amedhamiria kumaliza unyama dhidi ya polisi, kuleta mabadiliko na kuhakikisha waliotekeleza maovu wanawajibishwa.

Maandamano hayo yalitaka kikosi hicho kuvunjwa badala ya kufanyiwa marekebisho kwasababu malengo ya awali ya kubadilisha kikosi cha polisi hayakufanikiwa.

1px transparent line

Mara ya kwanza hatua hiyo ilionekana kama kile kilichokuwa kinatakiwa na waandamanaji: kuvunjwa kwa kikosi hicho maalum cha kupambana na uhalifu ambacho kilikuwa kimeshtumiwa kwa unyanyasaji wa haki za binadamu kwa miaka mingi.

Lakini kuna yale yanayotia hofu. Kuvunjwa kwa kikosi cha polisi cha Sars kunawadia kukiwa na hitaji moja maalum: Maafisa kutoka kikosi hicho chenye utata watahamishwa kwingineko. Bado haijafahamika watapelekwa wapi. Hilo ni muhimu kwasababu ingawa maandamano hayo yalianza kwa kutaka kundi hilo kuvunjwa, adai yamepanuka na kujumuisha kikosi cha polisi cha Nigeria kwa ujumla.

2px presentational grey line

Wanaharakati walisema kwa haraka kwamba unyanyasaji uliotekelezwa wakati wa maandamano ikiwemo kupigwa, vitisho na utumiaji wa nguvu kupita kiasi wakati wanakabiliana na maandamano hayo, yote hayo yalitekelezwa na maafisa wa polisi ambao hawakuwa wa kikosi cha Sars.

Kwao, kile kilichohitajika ni mabadiliko katika kikosi cha polisi kikamilifu nchini Nigeria. Bado haijabainika ikiwa kuna maafisa ambao wanashtakiwa kwa unyanyasaji wa siku za nyuma, jambo ambalo kundi la Amnesty International limesema ni muhimu kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika wote.

2px presentational grey line

Maandamano yame sambaakwa kiasi gani?

Wanahabari wa BBC nchini Nigeria wanasema kuwa mapigano kati ya waandamanaji wanaopinga kikosi hicho cha polisi cha Sars na maafisa wa polisi yamekuwa yakiendelea.

Watu kadhaa walioshuhudia wameiambia BBC wamepigwa na maafisa wa polisi pamoja na kutazama wengine wakishambuliwa wakati wa maandamano yaliotokea Jumapili, mwanahabari wa BBC nchini Nigeria Mayeni Jones amesema.

Mwanamke kijana aliyekuwa akitazama moja ya maandamano yanavyoendelea, ameiambia BBC kwamba alipigwa na maafisa 10 wa polisi ambao walivunja miwani yake. Mwanahabari wa BBC pia alisimamishwa na polisi na simu yake ya mkononi ikavunjwa na afisa mmoja.

police fire tear gas in abuja, 11/10

1px transparent line

Wakati huohuo, kumekuwa na hashtag ya #EndSARS inayosambaa mtandaoni kote nchini Nigeria na duniani, huku maandamano yakisambaa hadi Uingereza na Canada.

Watu maarufu nchini Nigeria ikiwemo wanamuziki Wizkid na Davido, pamoja na nyota wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria mwigizaji wa filamu za vita John Boyega, ameunga mkono maandamano hayo katika mitandao ya kijamii.

Jumapili waandamanaji ikiwemo Wizkid waliandamana katikati ya London.

Akihutubia waliondamana alisema vuguvugu jipya la maandamano linaashiria “Nigeria mpya” ambayo watu “hawataogopa kuzungumza wanachofikiria”.

“Vijana wa Nigeria musiache mtu yeyote awakataza kupaza sauti zenu. Tumefikia lengo letu – lakini huu ni wanzo tu,” alisema.

Maandamano ya hivi karibuni yalisababishwa na video ilionesha maafisa wa polisi wakiwatoa wanaume wawili kwa nguvu kutoka kwenye hoteli moja katika mji wa Lagos na kumpiga risasi mmoja wao.

Video hiyo ilivuja kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha hasira huku wengi wakishirikisha wengine simulizi za unyanyasaji zilizotekelezwa na kikosi hicho na kuonesha picha mbaya ya kunyanyasa vijana, mwanahabari wa BBC Nduka Orjinmo kutoka Abuja amesema.

Mapema mwaka huu kundi la Amnesty lilisema kwamba limesajili visa karibu 82 vya mateso yanayodaiwa kutekelezwa na kikosi hicho na mauaji ya kiholela kati ya Januari 2017 na Mei mwaka huu.

Idadi kubwa ya walioathirika walikuwa wanaume kati ya umri wa miaka 18 na 35 kutoka familia maskini na makundi yaliyo katika hatari. Wengi wa walioteswa walipigwa kwa fimbo na mapanga.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *