Polisi Waamua Kukesha na Msafara wa Tundu Lissu

October 7, 2020

 

Jeshi la polisi nchini limesema kuwa litakesha na Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA), Tundu Lissu kwani ni moja ya kazi yao wakiwa lindo.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa baada ya Lissu kutoa uamuzi wake wakubaki eneo ambalo msafara wake umezuiwa na polisi hadi utaratibu utapoeleweka.

“Lissu amesema atakaa pale,atalala pale,tunasema asante sana ,na sisi tutakesha nae pale,ni sehemu ya kazi yetu kukesha kwenye malindo’’alisema RPC Wankyo Nyigesa.

Aidha RPC Nyigesa ameweka bayana sababu yakuzuia msafara wa Lissu kuwa walihofia usalama wake kwani ameshazuiwa kufanya kampeni za urais kwa siku saba.

Taarifa ya CHADEMA ilisema kuwa msafara wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya Urais, Tundu Lissu, ulizuiliwa maeneo ya Kiluvya ukiwa unaeleka Kibaha.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *