Polisi ‘Tunamshikilia MTU mmoja Kati ya 17 Waliovamia Studio ya S2Kizzy Usiku

October 15, 2020

Polisi Kanda Maalum DSM wanamshikilia Mtu mmoja kati ya 17 waliovamia Studio ya @s2kizzy kwa kujifanya Polisi jamii na ulinzi shirikishi usiku wa October 14, 2020 ambapo waliwakamata Wasani na kuwapeleka Polisi kituo cha kijitonyama na kuwafungulia kesi za uongo.

“Nimeagiza Wasanii hao waliokamatwa waachiwe huru mara moja na hilo Genge  la wahuni lisakwe, hao sio Polisi Jamii, hakuna Polisi Jamii wanaoweza kufanya kazi peke yao bila Baraka za Viongozi wa Serikali, nimeagiza wahusika wote 17 wakamatwe, Kiongozi wao tunae na msako unaendelea”- MAMBOSASA   

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *