Polisi Belarus yatumia maji ya kuwasha, yawakamata waandamanaji,

October 4, 2020

 

Polisi nchini Belarus leo imetumia maji ya kuwasha kutawanya maandamano mjini Minsk huku maelfu ya waandamanaji wakiandamana katika mitaa ya mji huo katika maandamano ya hivi hivi karibuni dhidi ya rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko ambaye kuchaguliwa kwake tena kumekumbwa na utata.Waandamanaji hao wamesema maandamano hayo ni kuangazia masaibu ya wafungwa wa kisiasa. 

Maandamano hayo yamejiri baada ya Ubelgiji na Marekani kuweka vikwazo dhidi ya maafisa kadhaa wa wa Belarus. Lakini baada ya maandamano hayo kuanza katikati ya mji huo mkuu, polisi ilithibitisha kuyatawanya ikisema yalikuwa kinyume cha sheria. 

Msemaji wa wizara ya ndani Olga Chemodanova ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wamewakamata baadhi ya watu, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi.Kabla ya maandamano hayo, maafisa nchini humo waliondoa idhini kwa waandishi wa habari wote wa kigeni nchini humo hivyo kutatiza upeperushaji wa habari za maandamano ya upinzani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *