Paul Rusesabagina anyimya dhamana na korti ya Rwanda

September 18, 2020

Mahakama ya Rwanda imemnyima dhamana Paul Rusesabagina, aliyepata umaarufu kupitia filamu ya Hotel Rwanda, kwa kusema mashtaka ya ugaidi na mengine dhidi yake ni mazito na kuwa anapaswa kusalia kizuizini kwa siku nyengine 30.Rusesabagina, raia wa Ubelgiji na ambaye ana cha kuishi Marekani amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, alishtakiwa wiki hii kwa makosa 13 ikiwemo kosa la kufadhili ugaidi, mauaji, kutumikisha watoto kijeshi na kuunda kikundi cha waasi.Iwapo atapatikana na hatua, huenda akapewa kifungo cha miaka 25 gerezani. Hata hivyo, haijajulikana kesi yake itaanza lini. Akiongea na gazeti la Marekani la New York Times mbele ya maafisa wa Rwanda, Rusesabagina mwenye umri wa miaka 66 amesema alidhani kuwa ndege alimokuwa ameabiri kutoka Dubai ilikuwa inaenda Burundi ambako alitarajiwa kuzungumza na makanisa nchini humo.Hata hivyo, mahakama ya Rwanda imesema kuwa Rusesabagina alikamatwa katika uwanja wa kimataifa wa Kigali, taarifa hiyo ikiwa kinyume na iliyotolewa na polisi kuwa alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa.,

Mahakama ya Rwanda imemnyima dhamana Paul Rusesabagina, aliyepata umaarufu kupitia filamu ya Hotel Rwanda, kwa kusema mashtaka ya ugaidi na mengine dhidi yake ni mazito na kuwa anapaswa kusalia kizuizini kwa siku nyengine 30.

Rusesabagina, raia wa Ubelgiji na ambaye ana cha kuishi Marekani amekuwa mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, alishtakiwa wiki hii kwa makosa 13 ikiwemo kosa la kufadhili ugaidi, mauaji, kutumikisha watoto kijeshi na kuunda kikundi cha waasi.

Iwapo atapatikana na hatua, huenda akapewa kifungo cha miaka 25 gerezani. Hata hivyo, haijajulikana kesi yake itaanza lini. 

Akiongea na gazeti la Marekani la New York Times mbele ya maafisa wa Rwanda, Rusesabagina mwenye umri wa miaka 66 amesema alidhani kuwa ndege alimokuwa ameabiri kutoka Dubai ilikuwa inaenda Burundi ambako alitarajiwa kuzungumza na makanisa nchini humo.

Hata hivyo, mahakama ya Rwanda imesema kuwa Rusesabagina alikamatwa katika uwanja wa kimataifa wa Kigali, taarifa hiyo ikiwa kinyume na iliyotolewa na polisi kuwa alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *