Paul Rusesabagina adaiwa ‘kunyimwa’ wakili halisi, huku Kagame akisema lazima ajibu tuhuma dhidi yake

September 7, 2020

Dakika 1 iliyopita

Paul Rusesabagina

Baraza la kimataifa kuhusu msaada wa kibinadamu nchini Rwanda limekana madai kwamba kuna wakili aliyechaguliwa kumwakilisha mpinzani wa rais wa Rwanda Paul Rusesabagina.

Rusesabagina amekuwa akizuiliwa kwa siku tisa sasa tangu alipodaiwa kutekwa Dubai tarehe 28 Agosti .

”Kwa siku kadhaa , wakili anayemwakilisha Rusesabagina nchini Rwanda amezuiwa kumuona mteja wake”, ilisema ripoti hiyo.

Ripoti ya baraza hili inasema jana mtu asiyejulikana kwa familia ya Rusesabagina alifanya kikao na vyombo vya habari akisema kwamba ndie anayemwakilisha mshukiwa huyo.

Hatahivyo baraza hilo limekataa katakata kuhusu uwakilishi huo likisema kwamba hiyo ni njia moja ya ukiukaji wa haki ambao jamii ya kimataifa haifai kuvumilia.

Akizungumza mara ya kwanza kuhusu kukamatwa kwake, Rais wa Rwanda Paul Kagame Jumapili alisema kwamba Paul Rusesabagina hakutekwa, alidanganywa akajileta mwenyewe nchini Rwanda.

Rais Kagame alisema kwamba lazima Rusesabagina awajibishwe kuhusu mauaji dhidi ya raia wa Rwanda kufuatia mashambulio ya makundi ya waasi anayoongoza yaliyofanywa dhidi ya maeneo ya Rwanda miaka miwili iliyopita.

”Kumamatwa kwa Rusesababiga ambaye ni mmoja wa waliopanga mashambulio yaliyotoka Burundi ni moja ya njia ya kutekeleza hayo uliyoyasema kwamba unataka haki itendeke kwako na kwa wengine waliopoteza wame na mali zao, hatuwezi kukurusidia mume, lakini kile tunachoweza kukifanya ni kuhakikisha unapata haki yako ya kisheria”, Rais Kagame alimjibu mmoja wa wanawake waliomuuliza kwa njia ya simu kupitia televisheni kuhusu ni vipi anaweza kumsaidia baada ya kifo cha mume wake ambaye aliuawa katika mashambulio.

Baraza la kimataifa la Haki za binadmu kwa ajili ya Rwanda linadai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ana uraia wa Ubelgiji amenyimwa haki ya kutembelewa na ubalozi wan chi hiyo, Shirika la msalaba mwekundu mbali na kwamba pia hawezi kuwasiliana na familia yake.

Familia ya Rusesabaginaimewachagua mawakili 6 wataalamu wa sheria za kimataifa za haki za kibinadamu kumuwakilisha katika kesi inayomkabili nchini Rwanda, kutoka Rwanda, Ubelgiji, Astralia, Marekani na Canada.

Rusesabagina alifahamika kufuatia filamu ya Hotel Rwanda ikielezea jinsi alivyookoa maisha ya watutsi waliokuwa wamekimbilia katika hoteli moja mjini Kigali aliyokuwa meneja wake mwaka 1994.

Rais Paul Kagame amesema kikubwa sio ushujaa wa Bwana Rusesabagina au vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari akisema kinachoangaliwa kwa sasa ni yeye.

kuwajibishwa kuhusu kwa vitendo alivyotaja kuwa vya mauaji dhidi ya raia wa Rwanda.

Bwana Kagame amesema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ”hilo si jambo ambalo litakalomkabili mahakamani”.

“Kuna maswali ambayo lazima atayajibu.kuna wanaomsaidia wakiwa Ulaya,Marekani na kwIngineko na ambao walimpandisha cheo na kumpa majina ya ushujaa.awe shujaa au la ,mimi sina wasi wasi na hilo.

”Kikubwa tunachoangalia hapa ni kuhusika kwake na mauaji dhidi ya wa raia wa Rwanda, damu ya wananchi wa Rwanda iliyoko mikononi mwake kutokana na yeye kuongoza makundi ya kigaidi, lazima atawajibishwa kwa hayo” Alisema Rais Kagame.

Bwana Kagame amesema kuwa Paul Rusesabagina alikuwa kiongozi wa makundi ya watu wenye silaha, FNL miongoni mwao, na ambapo hivi karibuni lilianzisha mshambulizi dhidi ya Rwanda na ”kuua watu Kusini Magharibi”.

” Rusesabagina ametoa maelezo kabla hajafika hapa, mwenyewe akisifia jambo hilo.” Rais Kagame alisema.

Paul Rusesabagina, ni kiongozi wa muungano wa kisasa MRCD-Ubumwe ambacho Rwanda inauhusisha na mashambulio ya ugaidi yaliyowaua Wanyarwanda katika kituo cha polisi cha mjini Kigali.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, Reuters Baraza la kimataifa kuhusu msaada wa kibinadamu nchini Rwanda limekana madai kwamba kuna…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *