Paul Pogba: ‘Ni ndoto yangu kuichezea Real Madrid’

October 9, 2020

Dakika 7 zilizopita

Paul Pogba alifunga katika mechi ya hivi karibuni ya raundi ya nne ya kombe la Carabao

Maelezo ya picha,

Paul Pogba alifunga katika mechi ya hivi karibuni ya raundi ya nne ya kombe la Carabao

Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba amekiri kwamba ni ndoto yake kuichezea klabu ya Real Madrid siku moja.

Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliongezea kwamba atatumia kila njia kuiweka Man United pale inapotaka kuwa.

Kiungo huyo wa Ufarana amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kuondoka katika timu aliojiunga nayo kwa mara ya pili kwa dau la £89m mwaka 2016.

Kandarasi ya mshindi huyo wa kombe la dunia inaisha msimu ujao

Ijapokuwa United ina haki ya kumuongezea kandarasi ya mwaka mmoja. Na Pogba amesema kwamba hajakuwa na mazungumzo yoyote na klabu hiyo kuhusu kuongeza kandarasi yake.

”Hakuna mtu aliyeniambia chochote”, alisema katika mkutano na wanahabari akiwa na kikosi cha timu ya Ufaransa siku ya Alhamisi.

”Sijazungumza na afisa mkuu mtendaji Ed Woodward . hatujazungumza kuhusu mkataba mpya”.

”Kwa sasa niko katika klbau ya Man United na najaribu kuimarisha mchezo wangu. Najua kuna wakati ambapo klabu itanifuata na kuzungumza nami na pengine kuniwasilishia ombi fulani au la”.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kujiunga na klabu ya Real Madrid ambayo amekuwa akihusishwa nayo , alijibu

”Wachezaji wote wangependelea kuichezea Real Madrid , ni ndoto yangu , kwanini siku moja nisijiunge nao?” ,

”Nipo Man United na naipenda klabu yangu, Nachezea Man United , na nataka kuiweka klabu hii inapohitajika kuwa”.

United imeanza vibaya ligi msimu huu ikishinda mara moja katika mechi tatu.

Pogba ameanzishwa katika mechi zote msimu huu baada ya kujitenga alipoambukizwa virusi vya corona mwezi Agosti.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *