Patrice Lumumba: Mahakama ya Ubelgiji yasema jino la shujaa huyo wa DRC linapaswa kurudishwa

September 11, 2020

Dakika 2 zilizopita

Patrice Lumumba aliuawa 1961

Maelezo ya picha,

Patrice Lumumba aliuawa 1961

Mahakama mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino lililochukuliwa kutoka kwa maiti ya shujaa wa Uhuru wa taifa la DRC wakati huo ikiitwa Congo Patrice Lumumba linapaswa kurejeshwa kwa familia yao, vyombo vya habari nchini Ubelgiji vimeripoti.

Lumumba aliyekuwa waziri mkuu wa Congo baada ya kujipatia Uhuru kutoka kwa Ubelgiji 1960, aliuawa 1961 baada ya kutekwa na wapiganaji waliotaka kujitenga.

Serikali ya Ubelgiji ilihusika katika kifo chake na mwaka 2002 iliomba msamaha rasmi.

Vitengo vya ujasusi vya Uingereza na Marekani pia vinadaiwa kuhusika.

Jino la Lumumbua linadaiwa kuchukuliwa na afisa wa polisi wa Ubelgiji aliyekuwa anasaidia kuuzika mwili wake , chombo cha habari cha AFP kimeripoti.

Baadaye jino hilo lilichukuliwa na mamlaka ya Ubelgiji , AFP kinaongezea.

Mahakama hiyo ya Ubelgiji ilisema kwamba jino hilo sasa linafaa kupewa mwana wa kike wa Lumumba Juliana Lumumba , ambaye aliandika barua kwa mfalme huyo wa Ubelgiji akiomba lirudishwe, mtandao wa Brussels Times uliripoti.

Kulingana na mtandao huo uamuzi huo wa mahakama siku ya Alhamisi unafuatia uamuzi mwengine wa ofisi ya kiongozoi wa mashtaka wa kijimbo kwamba mabaki ya Lumumba yanaweza kurudishwa kwa familia yake,

kulingana na chombo cha habari cha Belga News.

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, AFP Maelezo ya picha, Patrice Lumumba aliuawa 1961 Mahakama mjini Ubelgiji imeamuru kwamba jino…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *