Paris yatangaza tahadhari ya juu ya COVID-19,

October 5, 2020

Jiji la Paris nchini Ufaransa limetangaza ”kiwango cha juu cha tahadhari” kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona. 

Hii inamaanisha kuwa hatua kali zinaanza kutekelezwa kuanzia leo Jumatatu, kama ilivyotangazwa na ofisi ya Waziri Mkuu wa Ufaransa, Jean Castex. 

Baa kwenye mji huo pamoja na vitongoji vyake zitafungwa na migahawa itaruhusiwa kufunguliwa endapo itazingatia masharti ya usafi. Aidha, mgombea urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden hajaambukizwa virusi vya corona. 

Timu yake ya kampeni imetangaza jana baada ya Biden kupimwa tena ugonjwa wa COVID-19. Huko Mexico, serikali imethibitisha kuongezeka kwa maambukizi hayo na kufikia 761,665 hapo jana, baada ya kutangaza visa vipya 3,712 na vifo zaidi 208. 

Naye Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Ardern amesema vizuizi vyote vya virusi vya corona kwenye mji wa Auckland vitaondolewa Oktoba 7.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *