Pakistan yakosolewa kwa mauaji ya waandishi, on September 8, 2020 at 6:00 pm

September 8, 2020

Umoja wa Mataifa umesema umeshtushwa na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari nchini Pakistan, ambayo mara nyingi hufanywa chini ya visingizio vya kukufuru na kuitusi dini. Umoja huo umeiagiza Pakistan kuchunguza vitisho vinavyowakabili waandishi hao.Umoja wa Mataifa umesema wasiwasi unaongezeka kutokana na maudhui ya ghasia na vitisho yanayowekwa mtandaoni na nje ya mitandao, aghalabu yakiwalenga waandishi wa habari wa kike na wanaharakati.Mmoja wa wahanga wa ghasia hizo hivi karibuni ni Shaheena Shaheen, aliyeuawa Jumamosi iliyopita katika jimbo la Balochistan, na wanaume ambao bado hawajakamatwa. Mwaka uliopita waandishi wa habari wanne waliuawa nchini Pakistan, kwa sababu zinazohusiana moja kwa moja na kazi wanayoifanya.Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Rupert Colville amesema wengi wa wale walioufanya uhalifu huo, kamwe hawafikishwi mbele ya mahakama.,

Umoja wa Mataifa umesema umeshtushwa na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari nchini Pakistan, ambayo mara nyingi hufanywa chini ya visingizio vya kukufuru na kuitusi dini. Umoja huo umeiagiza Pakistan kuchunguza vitisho vinavyowakabili waandishi hao.

Umoja wa Mataifa umesema wasiwasi unaongezeka kutokana na maudhui ya ghasia na vitisho yanayowekwa mtandaoni na nje ya mitandao, aghalabu yakiwalenga waandishi wa habari wa kike na wanaharakati.

Mmoja wa wahanga wa ghasia hizo hivi karibuni ni Shaheena Shaheen, aliyeuawa Jumamosi iliyopita katika jimbo la Balochistan, na wanaume ambao bado hawajakamatwa. Mwaka uliopita waandishi wa habari wanne waliuawa nchini Pakistan, kwa sababu zinazohusiana moja kwa moja na kazi wanayoifanya.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Rupert Colville amesema wengi wa wale walioufanya uhalifu huo, kamwe hawafikishwi mbele ya mahakama.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *