Pakistan yaishumu India kumuuwa askari wake na kuwajeruhi raia, on September 10, 2020 at 1:00 pm

September 10, 2020

 Jeshi la Pakistan limesema kuwa mwanajeshi wake mmoja ameuawa na raia watatu wamejeruhiwa katika makabiliano na wanajeshi wa India kwenye jimbo linalozozaniwa la Kashmir. Taarifa ya jeshi hilo imesema wanajeshi wa India wametumia silaha nzito kuwashambulia raia vijijini usiku wa kuamkia leo. Hayo yametokea kwenye mstari unaochukuliwa kama mpaka wa ushawishi kati ya India na Pakistan katika jimbo la Kashmir, ambalo kila upande unadai kulimiliki lote. Pakistan imetangaza vile vile kuwa imekidungua chombo cha anga cha upelelezi cha India, ambacho Pakistan imedai kiliingia katika anga lake. Nchi hizo hasimu zenye silaha za nyuklia zimekwishapigana vita mara mbili katika eneo hilo lililo katika bonde la Himalaya. Agosti mwaka uliopita, India ililipokonya eneo lake la Kashmir hadhi maalumu ya kujitawala, uamuzi uliofuatia na mivutano na mashambulizi ya hapa na pale.,

 

Jeshi la Pakistan limesema kuwa mwanajeshi wake mmoja ameuawa na raia watatu wamejeruhiwa katika makabiliano na wanajeshi wa India kwenye jimbo linalozozaniwa la Kashmir.

 Taarifa ya jeshi hilo imesema wanajeshi wa India wametumia silaha nzito kuwashambulia raia vijijini usiku wa kuamkia leo. 

Hayo yametokea kwenye mstari unaochukuliwa kama mpaka wa ushawishi kati ya India na Pakistan katika jimbo la Kashmir, ambalo kila upande unadai kulimiliki lote. 

Pakistan imetangaza vile vile kuwa imekidungua chombo cha anga cha upelelezi cha India, ambacho Pakistan imedai kiliingia katika anga lake. 

Nchi hizo hasimu zenye silaha za nyuklia zimekwishapigana vita mara mbili katika eneo hilo lililo katika bonde la Himalaya. 

Agosti mwaka uliopita, India ililipokonya eneo lake la Kashmir hadhi maalumu ya kujitawala, uamuzi uliofuatia na mivutano na mashambulizi ya hapa na pale.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *