, on September 10, 2020 at 5:00 pm

September 10, 2020

Mgombea Urais kupitia Chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa iwapo Watanzania watawapa ridhaa ya kuwaongoza watahakikisha wanafanya uchunguzi wa kina wa matukio mbalimbali ikiwemo yale yaliyofanywa na watu wasiojulikana ili kuwabaini.Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 10, 2020, wakati akifanya kampeni za kuomba kura za Urais na kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani katika jimbo la Kibiti, mkoani Pwani, ambapo amesema masuala ya haki za binadamu yataheshiniwa iwapo Watanzania wataondoa uwoga.”Watanzania tuchague watu waadilifu na wenye mapenzi na binadamu wenzao, tupambane na ugaidi na siyo kuvunja haki za binadamu watu wengi wamepotea bila kujulikana walipo, baadhi ya Watanzania wengine wamepata athari ya kupotelewa na ndugu zao hili si sahihi tunapaswa kuondoa uwoga ndani yetu ili kukomesha hali hii”, amesema profesa Lipumba.Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali kurithishana madaraka kwa watoto wao, na kusahau kuwa Watanzania pekee ndiyo wenye nafasi ya kuchagua kiongozi anayeweza kuwaletea maendeleo kwa maslahi yao.,

Mgombea Urais kupitia Chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa iwapo Watanzania watawapa ridhaa ya kuwaongoza watahakikisha wanafanya uchunguzi wa kina wa matukio mbalimbali ikiwemo yale yaliyofanywa na watu wasiojulikana ili kuwabaini.

Profesa Lipumba ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 10, 2020, wakati akifanya kampeni za kuomba kura za Urais na kuwanadi wagombea Ubunge na Udiwani katika jimbo la Kibiti, mkoani Pwani, ambapo amesema masuala ya haki za binadamu yataheshiniwa iwapo Watanzania wataondoa uwoga.

”Watanzania tuchague watu waadilifu na wenye mapenzi na binadamu wenzao, tupambane na ugaidi na siyo kuvunja haki za binadamu watu wengi wamepotea bila kujulikana walipo, baadhi ya Watanzania wengine wamepata athari ya kupotelewa na ndugu zao hili si sahihi tunapaswa kuondoa uwoga ndani yetu ili kukomesha hali hii”, amesema profesa Lipumba.

Katika hatua nyingine, Profesa Lipumba amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa Serikali kurithishana madaraka kwa watoto wao, na kusahau kuwa Watanzania pekee ndiyo wenye nafasi ya kuchagua kiongozi anayeweza kuwaletea maendeleo kwa maslahi yao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *