Ofisi ya Serikali Kidai kuwa Zahanati ya muda,

October 5, 2020

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani Michael Mwakamo, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi CCM kikishinda Oktoba 28 na kushika nafasi hiyo, atabadilisha matumizi ya Ofisi ya Kijiji cha Kidai kuwa Zahanati ya muda.

Mwakamo ametoa kauli hiyo kijijini hapo, ukiwa mkutani wake wa 25 ndani ya Kata ya Kikongo alipofanya mikutano miwili kikowemo Kijiji cha Mwanabwito, ambapo alisema kutokana na ukubwa wa jengo hilo, wakati wananchi wanatembea umbali mrefu kwemda kufuata huduma Mlandizi, ni vema likatumika kwa muda wakati utaratibu wa kujenga zahanati ukiendelea.

Mwakamo ameyasema hayo mwishoni mwa wiki kijijini hapo kwenye Mkutano wa 25 wa Kampeni ya kukiombea kura chama hicho, kuanzia rais Dkt. John Magufuli, ubunge na udiwani kwa Fatma Ngozi na wengine kutoka Kata 14 na wa Viti Maalumu wanaotokea chama hicho.

“Kwanza niwapongeze kwa ujenzi wa ofisi ya kisasa chini ya Mwenyekiti wenu Samson Masunzu, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa ofisi ya kisasa, kutokana na ukubwa wa jengo na shida ya huduma ya afya tunayoifuata Mlandizi, mikikichagua Chama Cha Mapinduzi nami ubunge tutabadili matumizi ya ofisi kuwa zahanati ya muda,” alisema Mwakamo.

Aliongeza kuwa akifanikiwa hilo atazungumza na Mganga Mkuu (DMO) ili wapatikane Daktari na wauguzi waanze kuwahudumia wananchi was maeneo hayo, huku wakifanya mchakato wa ujenzi wa zahanati, wakati Mwenyekiti akitafutiwa chumba kimoja cha ofisi.

“Hivi Mwenyekiti kwa ukubwa wa jengo lile kukaa kwa shughuli hizo, na kuligeuza zahanati ya muda unaonaje, au wananchi mnasemaje kuhusiana na ushauri huu? Lakini mazuri hayo yatafanyika mkimchagua Dkt. John Magufuli kuwa rais, Mwakamo Mbunge na Fatma Ngozi diwani,” alisema Mwakamo

Akizungumzia kero ya barabara ukanda wa Ruvu wenye kidongo cha mfinyanzi, Mwakamo alisema kuwa tatizo hilo litabaki historia, huku akieleza kwamba watakaa na TARURA watakapopewa  barabara za kuchonga mfano kilometa 70, watachonga nusu na kuweka kifusi tofauti na sasa ambapo wanachonga tu.

“Kwa utaratibu huo barabara zetu zitaimarika zaidi, kwa sasa TARURA wakipatiwa barabara za kuchonga hawaweki hata kifusi, kutokana na mfinyanzu uliopo mvua kidogo hazipitiki, tunakwenda kulipatia tiba tatizo hilo,” alisema Mwakamo.

Kwa upande wake Ngozi alimwambia mgombea huyo kwamba tatizo kubwa lililopo barabara hizo zinachongwa kipindi kinachokaribia masika, hivyo kusababisha kutodumu hali inayoongeza adha kwa wananchi wa maeneo hayo.

“Wananchi wanalalamikia kitendo cha kuchongwa barabara hizo ambazo kidongo chake ni cha mfinyanzi, ambapo panaponyesha mvua kidogo ubovu unarudi vilevile,” alisema Ngozi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *