Nzi atawala mdahalo wa makamu marais Marekani,

October 8, 2020

Nzi aliyetawala mdahalo wa makamu wa marais MarekaniImage caption: Nzi aliyetawala mdahalo wa makamu wa marais Marekani

Ikiwa moja ya vipimo vya mafanikio ni umaarufu kwenye mitandao ya kijamii basi mdahalo wa makamu marais Marekani umechukua kikombe.

Licha ya wagombea hao kujitahidi kwa kila namna kwenye hoja zao, hakuna walichosema kilichoendana na watu waliokuwa wanawafuatilia kupitia mitandaoni kama ilivyokuwa kwa nzi aliyejitokeza ambaye hakukutarajiwa.

Kwa takriban dakika mbili, nzi alitua kwenye kichwa cha makamu rais Mike Pence na moja kwa moja akawa maarufu.

Neno ‘nzi’ limesambaa kwenye mtandao wa Twitter zaidi ya mara 700,000 tangu alipojiteokeza wakati mdahalo unaendelea.

Kampeni ya Joe Biden nayo imetumia vizuri fursa hiyo kwa kusambaza maneno “flywillvote.com”.

Nzi huyo ameunganisha pande zote mbili huku mmoja akimpachika jina la “shujaa wa Marekani” na mwingine akisema “huenda ndio jambo litakalokumbukwa zaidi”.

Aidha, mmoja amelinganisha wakati wa mdahalo wa urais katika uchaguzi uliotanguliwa – miaka minne iliyopita ambapo nzi alijitokeza juu ya kichwa cha mgombea urais Hillary Clinton.

Hilo halimaanishi kwamba nzi huyo ni yule yule aliyejitokeza wakati huo na sasa amerejea tena.

Lakini sio wote waliomchukulia nzi huyo kwa utani kwasababu mchambuzi mwenye msimamo mkali Ben Shapiro alisema kuwa nzi huyo ni njia moja ya kutatiza kile kilichokuwa kinaendelea wakati wa mdahalo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *