Nyumba zaidi ya 1469 zaporoko kutokana na mafuriko nchini Indonesia, on September 14, 2020 at 10:00 am

September 14, 2020

Mvua kali zilizonyesha nchini Indonesia zimepelekea mafuriko ambayo pia yamesababisha  maporomoko ya ardhi.Majumba zaidi ya 1469  yameporomoko kwa maji kufuatia mvua kali ambazo zimenyesha katika kipindi hiki cha mvua za vuli.Eneo ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na mafuriko hayo ni eneo ambalo linapatikana Kaskazini mwa Kalimantan nchini humo.Kulingana na taarifa ambazo  zimetolewa na kitengo kinachohusika na misaada na uokozi katika matukio ya dharura, mvua kali zilizonyesha  katika eneo hilo zimesababisha mafuriko yaliopelekea uharibifu  hususan katika eneo la Melawi.Watu zaidi ya  5369 wameathirika na mafuriko hayo, ni mtu mmoja ndie ambae ameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko hayo.Zaidi ya familia 70 zimeondolewa katika eneo hilo abalo limefahamishwa kuwa ni hatari na kupelekwa katika eneo ambalo liliandaliwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.,

Mvua kali zilizonyesha nchini Indonesia zimepelekea mafuriko ambayo pia yamesababisha  maporomoko ya ardhi.

Majumba zaidi ya 1469  yameporomoko kwa maji kufuatia mvua kali ambazo zimenyesha katika kipindi hiki cha mvua za vuli.

Eneo ambalo limeathirika kwa kiasi kikubwa na mafuriko hayo ni eneo ambalo linapatikana Kaskazini mwa Kalimantan nchini humo.

Kulingana na taarifa ambazo  zimetolewa na kitengo kinachohusika na misaada na uokozi katika matukio ya dharura, mvua kali zilizonyesha  katika eneo hilo zimesababisha mafuriko yaliopelekea uharibifu  hususan katika eneo la Melawi.

Watu zaidi ya  5369 wameathirika na mafuriko hayo, ni mtu mmoja ndie ambae ameripotiwa kufariki kutokana na mafuriko hayo.

Zaidi ya familia 70 zimeondolewa katika eneo hilo abalo limefahamishwa kuwa ni hatari na kupelekwa katika eneo ambalo liliandaliwa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko hayo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *