Njombe:Serikali yaongeza muda vijana kuomba kujiunga na JKT, on September 8, 2020 at 6:00 pm

September 8, 2020

Na Amiri Kilagalila,NjombeSerikali Wilayani Njombe imeongeza muda wa siku nne kuanzia leo za kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga na nafasi za jeshi la kujenga Taifa (JKT) kutokana na vijana kutojitokeza kwa wingi mwaka huu.Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri amesema zoezi hilo  lilitakiwa kukamilika septemba 9 mwaka huu na kutokana na idadi ndogo ya vijana waliokwenda kuomba, serikali imeongeza muda huo wa siku nne hadi tarehe 11 .“Tarehe yetu ya mwisho ya kupokea tulikuwa tumepanga iwe tarehe 9 saa kumi jioni ambayo ni kesho,lakini mimi nimefungua na nitaendelea kupokea majina ya waombaji wote na vikao vyangu nitafunga rasmi tarehe 11”alisema Ruth MsafiriAidha Bi.Msafiri amesema vijana wenye sifa ya kujiunga na JKT ni wenye elimu ya darasa la saba hadi chuo kikuu ambapo vijana 130 wanahitajika kujiunga na jeshi hilo.“Kwa kuwa lengo ni kupata vijana wa kutosha kupata fani na stadi mbali mbali za maisha,hii inahusisha madarasa yote kwa maana elimu ya msingi,sekondari,kidato cha sita,cheti,lakini pia hata wa chuo kikuu”aliongeza DC MsafiriB.Msafiri ametumia fursa hiyo kukemea tabia za baadhi ya watu wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia zoezi hilo  kinyume na sheria ambapo kwa atakaye bainika hatua kali zitachukuliwa.“Hizi nafasi hazitolewa kwa upendeleo wa aina yeyote,wewe ukitoa rushwa utakuwa umeumizwa,mimi sitoi hiz nafasi kwa upendeleo kwasababu sio za mfukoni ila tunakwenda nazo kwa sifa”alisema Ruth MsafiriKituo hiki kimezungumza na baadhi ya vijana mjini Njombe wamesema wanatambua kuwepo umuhimu wa kujiunga na JKT ikiwemo kujengewa uzalendo na kulilinda Taifa.,

Na Amiri Kilagalila,Njombe
Serikali Wilayani Njombe imeongeza muda wa siku nne kuanzia leo za kutuma maombi kwa ajili ya kujiunga na nafasi za jeshi la kujenga Taifa (JKT) kutokana na vijana kutojitokeza kwa wingi mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Ruth Msafiri amesema zoezi hilo  lilitakiwa kukamilika septemba 9 mwaka huu na kutokana na idadi ndogo ya vijana waliokwenda kuomba, serikali imeongeza muda huo wa siku nne hadi tarehe 11 .

“Tarehe yetu ya mwisho ya kupokea tulikuwa tumepanga iwe tarehe 9 saa kumi jioni ambayo ni kesho,lakini mimi nimefungua na nitaendelea kupokea majina ya waombaji wote na vikao vyangu nitafunga rasmi tarehe 11”alisema Ruth Msafiri

Aidha Bi.Msafiri amesema vijana wenye sifa ya kujiunga na JKT ni wenye elimu ya darasa la saba hadi chuo kikuu ambapo vijana 130 wanahitajika kujiunga na jeshi hilo.

“Kwa kuwa lengo ni kupata vijana wa kutosha kupata fani na stadi mbali mbali za maisha,hii inahusisha madarasa yote kwa maana elimu ya msingi,sekondari,kidato cha sita,cheti,lakini pia hata wa chuo kikuu”aliongeza DC Msafiri

B.Msafiri ametumia fursa hiyo kukemea tabia za baadhi ya watu wanaotaka kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia zoezi hilo  kinyume na sheria ambapo kwa atakaye bainika hatua kali zitachukuliwa.

“Hizi nafasi hazitolewa kwa upendeleo wa aina yeyote,wewe ukitoa rushwa utakuwa umeumizwa,mimi sitoi hiz nafasi kwa upendeleo kwasababu sio za mfukoni ila tunakwenda nazo kwa sifa”alisema Ruth Msafiri

Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya vijana mjini Njombe wamesema wanatambua kuwepo umuhimu wa kujiunga na JKT ikiwemo kujengewa uzalendo na kulilinda Taifa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *