Nini Sarpong, Bocco ni Hatari Aisee…’

October 3, 2020

BEKI wa Mtibwa Sugar, Dickson Job, amefunguka kuwa mshambuliaji wa Simba, John Bocco ni hatari zaidi ya Mghana wa Yanga, Michael Sarpong.

Job msimu huu amecheza na mastraika hao kwa nyakati tofauti akiwa na uzi wa Mtibwa Sugar akishirikiana na pacha wake Jofrey Luseke.

Kwanza beki huyo alikutana na Bocco kwenye sare ya 1-1, kisha dhidi ya Yanga, Mtibwa ikafungwa 1-0. Mechi zote zilichezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Akizungumza na Spoti Xtra, Job alisema: “Msimu huu nimecheza dhidi ya Simba na Yanga, kwa upande wangu licha ya kwamba Yanga walifanikiwa kushinda, lakini naamini Simba wako bora zaidi hata kama hawakuweza kuibuka na ushindi.

“Lakini pia kama ningeambiwa nimtaje mshambuliaji ambaye aliisumbua sana safu yetu ya ulinzi kati ya wale wa Simba na Yanga basi Bocco alikuwa hatari zaidi kwetu kuliko hata yule Sarpong.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *