Nini kinachoendelea kuhusu uongozi wa chama tawala cha Kenya?, on September 20, 2020 at 3:00 pm

September 20, 2020

 Baada ya kuchaguliwa tena kuongoza kwa miaka mitano, jambo ambalo lilitokea baada ya kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wao na mahakama, Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamekuwa wakivuta kuelekea pande mbili tofauti.Kutengana kwao kulianza kuonekana baada ya mwezi wa Machi, 2018,(Rais Kenyatta alianza kuwa na uhusiano na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga) na baada ya hapo, kumekuwepo na shutuma kutoka pande mbili husika.Rais Kenyatta alimshutumu naibu wake kwa kushiriki katika kampeini za kisiasa za kumrithi mapema mno badala ya kulenga miradi waliyokuwa wameahidi Wakenya. Kwa upande mwingine, naibu Rais William Ruto anaiona hatua hii kama njama ya kumkata mikono katika kumrithi rais Uhuru na kwenda kinyume cha makubaliano yao ya mwaka wa 2013 ambayo yalifanywa wakati wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya jinai katika mahakama ya kimataifa(ICC).Katika chama cha Jubilee, uhusiano kati ya Rais Uhuru na naibu wake umekuwa unadorora. Chama cha Jubilee ambacho kiliundwa mnamo Septemba 2016 ili kuunda muungano kati ya Uhuru Kenyatta na Ruto sasa unadhibitiwa na Rais Kenyatta huku viongozi wake wengine wakuu, akiwemo Bw. Ruto wakiwa wameonekana kutengwa.Hali hii inatokana na siasa za ndani kwa ndani kwenye chama hicho tawala kuhusiana na suala la vita dhidi ya ufisadi, huku Rais Kenyatta akikumbwa na mgawanyiko katika siasa za Mlima Kenya, anakotoka Rais Kenyatta. Wafuasi wa Rais Kenyatta wamegawanyika; wengine wakimuunga mkono Bw. Ruto huku wengine wakimuunga mkono Rais Kenyatta.Haya yakiendelea, wanachama wa chama cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM) wamekuwa wakimtetea Rais Kenyatta kutokana na shutuma za wanajubilee. Kwa njia hii, Raila Odinga amekuwa mtetezi wa Rais Kenyatta huku Ruto akionekana kuongoza upinzani ndani ya chama tawala cha Jubilee.Kwa upande wake, Rais Kenyatta ameunda muungano mpya akitumia wapinzani wa kisiasa wa Ruto akimleta karibu kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa chama cha Orange Democratic Movement(ODM), kinara wa Wiper Democratic Movement (WDM) Kalonzo Musyoka, Gideon Moi wa Kanu na Isaac Ruto wa Chama Cha Mashinani.Ushirikiano huu na vyama vingine umesababisha fujo katika vyama vya upinzani nchini Kenya huku vyama vingine vikijaribu kusimama imara hasa katika ngome zao za kisiasa. Kwa mfano chama cha Ford-K kimekumbwa na migogoro ya kiusimamizi ya ndani kwa ndani na mpaka sasa kina viongozi wawili. Makundi mawili ya uongozi sasa yako mahakamani kupigania uongozi wa chama cha Fork-K.Hali hii ndiyo iliyopelekea Rais Kenyatta kuchukua usimamizi dhabiti wa bunge la kitaifa na lile la seneti ambapo kwa sasa mabunge haya hayana upande wa upinzani. Naibu wa Spika wa bunge la seneti, kiongozi wa wengi na kamati zake zimefanyiwa mabadiliko makubwa. Hali hii imekumba bunge la kitaifa ambapo kiongozi wa wengi na naibu wake na kamati zake pia zimefanyiwa mchujo. Hali hii mpya inatishia uhuru wa bunge katika utendakazi wake nchini Kenya.Miungano mipya katika siasa za Kenya ina misingi yake katika uhusiano kati ya Rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na huenda pia ikakumbwa na mitetemeko zaidi huku viongozi hawa wawili wakiweka mipango kwa kura ya maamuzi kuhusu katiba ya Kenya. Kampeini kuhusiana na jambo hili zilisambaratishwa na ugonjwa wa Covid-19 huku Rais Kenyatta na Raila Odinga wakisisitiza siku za hivi karibuni kuwa bado mipango ingalipo.Kwa naibu Rais William Ruto, kuondolewa kwa wandani wake katika nyadhifa mbali mbali kunamaanisha kuwa ni bayana kwamba makubaliano yake na Rais Kenyatta ya mwaka wa 2013 ambayo yangemfanya kumrithi Kenyatta kama rais wa tano wa Kenya, hayapo tena. Haya yakimaanisha kuwa ni lazima bwana Ruto apange mkakati mwingine.Ni bayana pia kwamba huenda akafaidika kutokana na kutoelewana kwa kundi kubwa lililoletwa pamoja na Rais Kenyatta. Mgogoro na uhusiano baina ya Rais Kenyatta na naibu wake huenda ukachacha zaidi iwapo mpango wa marekebisho ya katiba utaanza hivi karibuni. Bwana Ruto anatofautiana na Rais kuhusiana na jambo hili. Ruto anasema kwamba hakuna dharura katika kuifanyia marekebisho katiba ya Kenya na kwamba fikra ya kutaka kuipanua serikali hasa katika ngazi na nyadhifa za juu kupitia kwa marekebisho haya ni jambo lisilofaa.Wengi wanaamini kwamba Ruto amekasirishwa na kuvunjwa moyo baada ya kugundua kwamba Rais Kenyatta huenda asimuunge mkono katika uchaguzi wa 2022. Hali hii imepelekea maswali mengi kuibuka kama chama cha Jubilee kitakuwa imara hadi uchaguzi wa mwaka wa 2022. Kumekuwepo na minongono kwamba Bwana Ruto huenda akakihama chama hicho ambacho amedai hakina udhabiti na kimetekwa nyara na matapeli wa kisiasa.Bwana Ruto amedokeza pia kuwa huenda akaongoza upande utakaopinga kura ya maamuzi kuhusu katiba ya Kenya huku akikejeli wanaounga mkono suala hili. “Hata sijui ni nini kitakachobadilishwa…kulingana na ufahamu wangu, mabadiliko haya yanasukumwa na viongozi, si wananchi. Wananchi kwa sasa wanashughulishwa na ukosefu wa ajira, na mambo mengine ya kimsingi katika maisha yao.” Bwana Ruto amenukuliwa akisema.Kwa upande wake, Rais Kenyatta anasisitiza kwamba kura ya maamuzi ni lazima kufanyika ili kuondoa hali ya wasiwasi ambayo hukumba Kenya kila mara kabla na baada ya uchaguzi mkuu kwa sababu wa jamii fulani “kuhisi kutengwa kutoka kwa uongozi wa taifa” jambo linalopelekea uhasama baina na kati ya jamii.Rais Kenyata amekuwa akieleza kuwa ana maono ya kulipokeza taifa hali ya mshikamano na umoja kupitia mchakato wa BBI, ambao utakuwa sehemu ya jinsi atakavyokumbukwa akiondoka mamlakani.Lakini naibu wake anahoji kuwa mabadiliko ya kikatiba hayawezi kufanywa kuwa jinsi kiongozi yeyote atakavyokumbukwa. “Mabadiliko ya kikatiba si jambo tunaloweza kuamua kama chama- ni kwa Wakenya wote kuamua. Si jambo ambalo ninaweza kusema kwamba nitakumbukwa kwa kubadilisha katiba,” aliambia kituo kimoja cha televisheni nchini Kenya hivi maajuzi.,

 

Baada ya kuchaguliwa tena kuongoza kwa miaka mitano, jambo ambalo lilitokea baada ya kufutiliwa mbali kwa uchaguzi wao na mahakama, Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamekuwa wakivuta kuelekea pande mbili tofauti.

Kutengana kwao kulianza kuonekana baada ya mwezi wa Machi, 2018,(Rais Kenyatta alianza kuwa na uhusiano na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga) na baada ya hapo, kumekuwepo na shutuma kutoka pande mbili husika.

Rais Kenyatta alimshutumu naibu wake kwa kushiriki katika kampeini za kisiasa za kumrithi mapema mno badala ya kulenga miradi waliyokuwa wameahidi Wakenya. Kwa upande mwingine, naibu Rais William Ruto anaiona hatua hii kama njama ya kumkata mikono katika kumrithi rais Uhuru na kwenda kinyume cha makubaliano yao ya mwaka wa 2013 ambayo yalifanywa wakati wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa makosa ya jinai katika mahakama ya kimataifa(ICC).

Katika chama cha Jubilee, uhusiano kati ya Rais Uhuru na naibu wake umekuwa unadorora. Chama cha Jubilee ambacho kiliundwa mnamo Septemba 2016 ili kuunda muungano kati ya Uhuru Kenyatta na Ruto sasa unadhibitiwa na Rais Kenyatta huku viongozi wake wengine wakuu, akiwemo Bw. Ruto wakiwa wameonekana kutengwa.

Hali hii inatokana na siasa za ndani kwa ndani kwenye chama hicho tawala kuhusiana na suala la vita dhidi ya ufisadi, huku Rais Kenyatta akikumbwa na mgawanyiko katika siasa za Mlima Kenya, anakotoka Rais Kenyatta. Wafuasi wa Rais Kenyatta wamegawanyika; wengine wakimuunga mkono Bw. Ruto huku wengine wakimuunga mkono Rais Kenyatta.

Haya yakiendelea, wanachama wa chama cha upinzani Orange Democratic Movement (ODM) wamekuwa wakimtetea Rais Kenyatta kutokana na shutuma za wanajubilee. Kwa njia hii, Raila Odinga amekuwa mtetezi wa Rais Kenyatta huku Ruto akionekana kuongoza upinzani ndani ya chama tawala cha Jubilee.

Kwa upande wake, Rais Kenyatta ameunda muungano mpya akitumia wapinzani wa kisiasa wa Ruto akimleta karibu kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa chama cha Orange Democratic Movement(ODM), kinara wa Wiper Democratic Movement (WDM) Kalonzo Musyoka, Gideon Moi wa Kanu na Isaac Ruto wa Chama Cha Mashinani.

Ushirikiano huu na vyama vingine umesababisha fujo katika vyama vya upinzani nchini Kenya huku vyama vingine vikijaribu kusimama imara hasa katika ngome zao za kisiasa. Kwa mfano chama cha Ford-K kimekumbwa na migogoro ya kiusimamizi ya ndani kwa ndani na mpaka sasa kina viongozi wawili. Makundi mawili ya uongozi sasa yako mahakamani kupigania uongozi wa chama cha Fork-K.

Hali hii ndiyo iliyopelekea Rais Kenyatta kuchukua usimamizi dhabiti wa bunge la kitaifa na lile la seneti ambapo kwa sasa mabunge haya hayana upande wa upinzani. Naibu wa Spika wa bunge la seneti, kiongozi wa wengi na kamati zake zimefanyiwa mabadiliko makubwa. Hali hii imekumba bunge la kitaifa ambapo kiongozi wa wengi na naibu wake na kamati zake pia zimefanyiwa mchujo. Hali hii mpya inatishia uhuru wa bunge katika utendakazi wake nchini Kenya.

Miungano mipya katika siasa za Kenya ina misingi yake katika uhusiano kati ya Rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na huenda pia ikakumbwa na mitetemeko zaidi huku viongozi hawa wawili wakiweka mipango kwa kura ya maamuzi kuhusu katiba ya Kenya. Kampeini kuhusiana na jambo hili zilisambaratishwa na ugonjwa wa Covid-19 huku Rais Kenyatta na Raila Odinga wakisisitiza siku za hivi karibuni kuwa bado mipango ingalipo.

Kwa naibu Rais William Ruto, kuondolewa kwa wandani wake katika nyadhifa mbali mbali kunamaanisha kuwa ni bayana kwamba makubaliano yake na Rais Kenyatta ya mwaka wa 2013 ambayo yangemfanya kumrithi Kenyatta kama rais wa tano wa Kenya, hayapo tena. Haya yakimaanisha kuwa ni lazima bwana Ruto apange mkakati mwingine.

Ni bayana pia kwamba huenda akafaidika kutokana na kutoelewana kwa kundi kubwa lililoletwa pamoja na Rais Kenyatta. Mgogoro na uhusiano baina ya Rais Kenyatta na naibu wake huenda ukachacha zaidi iwapo mpango wa marekebisho ya katiba utaanza hivi karibuni. Bwana Ruto anatofautiana na Rais kuhusiana na jambo hili. Ruto anasema kwamba hakuna dharura katika kuifanyia marekebisho katiba ya Kenya na kwamba fikra ya kutaka kuipanua serikali hasa katika ngazi na nyadhifa za juu kupitia kwa marekebisho haya ni jambo lisilofaa.

Wengi wanaamini kwamba Ruto amekasirishwa na kuvunjwa moyo baada ya kugundua kwamba Rais Kenyatta huenda asimuunge mkono katika uchaguzi wa 2022. Hali hii imepelekea maswali mengi kuibuka kama chama cha Jubilee kitakuwa imara hadi uchaguzi wa mwaka wa 2022. Kumekuwepo na minongono kwamba Bwana Ruto huenda akakihama chama hicho ambacho amedai hakina udhabiti na kimetekwa nyara na matapeli wa kisiasa.

Bwana Ruto amedokeza pia kuwa huenda akaongoza upande utakaopinga kura ya maamuzi kuhusu katiba ya Kenya huku akikejeli wanaounga mkono suala hili. “Hata sijui ni nini kitakachobadilishwa…kulingana na ufahamu wangu, mabadiliko haya yanasukumwa na viongozi, si wananchi. Wananchi kwa sasa wanashughulishwa na ukosefu wa ajira, na mambo mengine ya kimsingi katika maisha yao.” Bwana Ruto amenukuliwa akisema.Kwa upande wake, Rais Kenyatta anasisitiza kwamba kura ya maamuzi ni lazima kufanyika ili kuondoa hali ya wasiwasi ambayo hukumba Kenya kila mara kabla na baada ya uchaguzi mkuu kwa sababu wa jamii fulani “kuhisi kutengwa kutoka kwa uongozi wa taifa” jambo linalopelekea uhasama baina na kati ya jamii.

Rais Kenyata amekuwa akieleza kuwa ana maono ya kulipokeza taifa hali ya mshikamano na umoja kupitia mchakato wa BBI, ambao utakuwa sehemu ya jinsi atakavyokumbukwa akiondoka mamlakani.

Lakini naibu wake anahoji kuwa mabadiliko ya kikatiba hayawezi kufanywa kuwa jinsi kiongozi yeyote atakavyokumbukwa. “Mabadiliko ya kikatiba si jambo tunaloweza kuamua kama chama- ni kwa Wakenya wote kuamua. Si jambo ambalo ninaweza kusema kwamba nitakumbukwa kwa kubadilisha katiba,” aliambia kituo kimoja cha televisheni nchini Kenya hivi maajuzi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *