Nigeria: Aliyewanyonga wanawake tisa ahukumiwa kifo,

October 10, 2020

Mwanaume aliyewaua wanawake tisa na kesi yake ikaibua ghadhabu amehukumiwa kunyongwa katika mjini wa kusini wa Port Harcourt.

Waendesha mashtaka wamesema mwanaume huyo, mwenye miaka 26, Gracious David-West aliwanyonga wanawake hao katika hoteli mbalimbali nchini Nigeria alikokuwa anakutana nao kati ya mwezi Julai na Septemba 2019

Jaji Adolphus Enebeli amesema kifo chake kitatekelezwa kwa kunyongwa. Hukumu hiyo ya kifo ni nadra sana kutolewa nchini Nigeria — hukumu ya kifo mara ya mwisho kutolewa ilikuwa ni mwaka 2016 kwa watu watatu.

Mmoja wa waathirika alinusurika na shambulio lake lakini hakuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi wakati kesi hiyo inaendelea.

Wakati wa mfululizo wa mauaji ya wanawake hao mwezi Septemba mwaka jana, raia wenye hasira waliandamana barabarani na kuitaka mamlaka kuchukua hatua kutatua tatizo hilo. Mtuhumiwa alikamatwa Septemba 19, wakati akijaribu kuondoka Port Harcourt wakati ambapo mamlaka ilikuwa karibu kumkuta na hatia.

Picha za video za CCTV zilimpiga picha akiwa anaondoka hotelini na picha hizo zilienea katika mitandao ya kijamii.

Watu wa usalama walimkuta katika basi akisafiri kutoka Uyo katika jimbo la Akwa Ibom , ambako ni mbali kutoka Port Harcourt kwa dakika 45.

David-Westa alizaliwa katika mji wa wavuvi wa jimbo la Buguma, eneo ambalo linafahamika sana kwa kutengeneza mafuta na fukwe zake kuwa za kuvutia.

Polisi wanasema David-West alikuwa mjumbe wa kikundi cha wanamgambo wa kigaidi kijulikanacho kama Greenlanders – au Dey Gbam.Wale waliomfahamu waliiambia BBC kuwa alikuwa mtoto wa pekee katika familia , ingawa mama yake na baba yake walikuwa wanaishi tofauti.

Waandishi waliomuona mahakamani walimuelezea tabia yake kuwa haieleweki.

“Alikuwa na hasira sana, alikuwa anamkatisha jaji kila mara na alikuwa anataka kujitetea mwenyewe licha ya kuwa na wakili,” alisema mwandishi Alwell Ene.

Alitimia hoteli za bei nafuu ambazo hazina usalama mzuri kama kuwa na kamera za CCTV, katikati ya mji wa Port Harcourt, kwa mujibu wa polisi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *