Ni kwanini maelfu ya wanawake wa Rwanda wamepewa ruhusa ya kuavya mimba?

September 20, 2020

Dakika 3 zilizopita

Uavyaji mimba

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Rwanda yanasema tangu kufanyiwa marerkebisho ya sheria ya kuavia mimba nchini Rwanda 2018 , hadi leo waliopewa ruhusa ya kutoa mimba ni takriban 150,000.

Mabadiliko hahyo yamewapa fursa wanawake waliopata mimba wakiwa na umri mdogo, waliobakwa, waliolazimishwa kuolewa, waliopewa mimba na ndugu zao wa damu pamoja na wenye mimba zinazoweza kuathiri afya ya mama na mtoto.

Wasichana wawili, mmoja mwenye umri wa miakqa 18, tunayemuita hivi karibuni walisaidiwa kuavia mimbachanga kwasababu walibakwa, walizungumza na Maria anasema alibakwa na wanaume watatu kwa mkupuo.

“Mtu tunayefahamiana aliniiya akiiniambia nije anipatie kazi, nilipoenda nikawakuta vijana watatuwakanibaka wote kwa pamoja.”, anasema.

Kwa upande wake Jeanne pia anasema alipachikwa mimba kupitia ubakaji:

“Lilikuwa ni jambo walilolipanga, walichukua soda wakaichanganya na pombe. Nilipomaliza kuinywa nilihisi kuna kitu kimebadilika mwilini mwangu , kwasababu nilikuwa sijawahi kunywa pombe maishani, sijui ni nini kilitokea baadae, ila kulipokucha nilijipata nikiwa na kijana huyo .”

Sawa na wasichana wengine wengi waliopata ujauzito kwa njia hiyo ya kubakwa, wasichana hawa waliogopa kuwaambia wazazi wao yaliyowasibu kutokana na namna wazazi wanavyopokea taarifa za kubakwa kwa watoto wao. Kwahiyo waliamjua kwenda katika mashirika ya kutetea haki za binadamu ili yawasaidie.

Health Development Initiative (HDI), Great Lakes Initiative for Human Rights na Development (GLIHD), Isange One Stop Center nha mashirika mengine huwasaidia wasichana wenye matatatizo ya aina hii kupata haki ya kuavya mimba.

Jeanne anasema kwamba kwa sasa anajihisi vyema baada ya kusaidiwa kuavya mimba wimbi mbili zilizopita.

Majuto

Maria na Jeanne wanasema kuwa kuavya mimba sio uamuzi rahisi hata kidogo
Maelezo ya picha,

Maria na Jeanne wanasema kuwa kuavya mimba sio uamuzi rahisi hata kidogo

Maria na Jeanne wanasema kuwa kuavya mimba sio uamuzi rahisi hata kidogo, kwasababu walipofanyiwa vipimo hospitalini walianza kuoneshwa jinsi mtoto anavyolingana tumboni mwao.

Wote wanasema kuna wakati wanahisi kujutia kitendo walichokifanya na kulazimika kuomba ushauri nasaha: “Kuna wakati ninajiuliza …labda ningeacha kuavya mimba ile huenda mtoto angekua… na baadaye sijui angekuwa mtu wa aina nani?’…lakini kwa upande mwingine najipatia moyo na kusema ‘sikuwa na chaguo jingine’.

“Huwa ninahisi ninahitaji mtu ambaye tunaweza kuzungumza nae aniambie ni vipi ninaweza kusahau, sio rahisi kusahau kuwa niliavya mimba, lakini hatimaye nitasahau.”

“Nilijihisi mwenye uoga fulani, na hata sasa kuna wakati ninawaza na ninahisi nilifanya dhambi kwa kiasi fulani, lakini kusema ukweli sikuwa na mahali pa kumpeleka huyo mtoto kwasababu sikufanya ngono kwa utashi wangu .” Jeanne anasema.

Lakini kwa ujumla wote wanafurahia kwamba sheria mpya iliwapa uwezo wa kuchagua zaidi ya kuzaa mtoto kwa njia ambayo hawakuipanga wala kuitaka.

Mimba
Maelezo ya picha,

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanalalamika baadhi ya madaktari wanakataa kuavya mimba kwasababu ya imani zao

Mashirika yanayotetea haki za binadamu nchini Rwanda yanasema bado kuna pingamizi katika utekelezwaji wa sheria hii, kama vile imani za kidini za watekelezaji ambao ni madaktari na wauguzi.

Aphrodis Kagaba mkuu wa shirika la haki za binadamu la HDI-Rwanda anasema: “Daktari anakwambia kwamba nikizingatia na imani yangu ya kidini na kanisa langu , mimi hiki kijtu cha kuavya mimba siwezi kukifanya. Lakini kama wewe ni daktari unatakiwa kuwatibu watu wote bila kuwatenga baadhi” anasema na kuongeza kuwa ” Jambo jingine ni jinsi huduma hizo za kuavya mimba zinavyopaswa kutolewa kwa siri, tunahitaji watu wapewe mafunzo kuwanzia wanaowapokea waathiriwa .”

Bwana Kagaba anasema nivyema aliyekubaliwa kisheria kuavya mimba apewe huduma nzuri ili asipatwe na madhara yoyote.

Vestine Husna Umulisa, naibu mkuu wa shirika la haki za binadamu la GLIHD, anasema tatizo jingine ni la uchache wa wanaume wanaoadhibiwa baada ya kuwapachika mimba watoto wa kike, huku vitendo hivyo vikiendelea kuongezeka.

Anasema : “Hadi leo kuna watoto wa kike 18,000 nwaliopachikwa mimba, wote wamekwishajifungua, lakini ni 3,000 waliokwisha fikishwa mbele ya waendesha mashitaka na kuadhibiwa.”Tunaiomba serikali ichukue hatua dhidi ya wanaume wanaowabebesha mimba watoto wadogo wa kike.”

Unaweza pia kusoma:

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, Getty Images Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Rwanda yanasema tangu kufanyiwa marerkebisho…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *