Ng’ombe wa Waziri Mpina warejeshwa RANCHI West Kilimanjaro, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 30, 2020 at 6:00 pm

August 30, 2020

Na Mwandishi Wetu, SihaAGIZO lililotolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kuhusiana na Kashfa ya Wizi wa ng’ombe 17 wenye thamani ya shilingi milioni 14 katika Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro limetekelezwa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu kukabidhiwa ng’ombe hao baada waliokuwa watumishi wa ranchi hiyo kununua wengine.Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, alisema ng’ombe  amekabidhiwa na Meneja wa Kampuni hiyo, Mbelwa Lutagwelera ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mpina aliyeagiza ngombe kurejeshwa kwenye ranchi na kukataa sababu zilizokuwa zimetolewa kuwa ng’ombe wameibiwa.“Ni kweli nimepokea leo ng’ombe hao baada ya kurejeshwa kama Mh Waziri alivyoagiza alipotembelea Ranchi hii kwamba mifugo hiyo ipatikane haraka na hatua ziendelee kuchukuliwa kwa wote waliohusika na kashfa hiyo”alisema Buswelu.Pia Mkuu huyo wa wilaya ameagiza Menejimenti ya NARCO kuajiri walinzi wenye sifa na hasa waliopitia mafunzo kutoka kutoka Jeshi la Akiba ambao wamefundishwa uadilifu na uzalendo wa nchi yao, badala ya kuajiri watu wasiokuwa na sifa.Buswelu aliwataka watumishi wa ranchi hiyo kusimamia ulinzi wa rasilimali za kampuni hiyo na kujiepusha na vitendo vya kuwa sehemu ya kuhujumu na kushiriki vitendo vya wizi na badala yake wazalishe ng’ombe wengi ili taifa lipate fedha nyingi kutokana na mifugo.Wakati Waziri Mpina alipotembelea Ranchi hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo aliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata kwa watumishi wote wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) West Kilimanjaro kufuatia kashfa ya kupotea kwenye Mazingira ya kutatanisha ng’ombe 17 wa Serikali waliokuwa wanatunzwa kwenye ranchi hiyo.Buselu amesema tangu wizi huo ufanywe hakuna taarifa yoyote iliyowasilishwa kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo jambo linaonesha kuna njama za makusudi zilizowekwa na watumishi hao kuiibia Serikali jambo ambalo halikubaliki.Hivi karibuni, Waziri wa Mifugo na Uvivi, Luhaga Mpina alipoitembelea wilaya hiyo, alieleza kutokuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Ranchi kuhusiana na kashfa hiyo na kuagiza kuwa ifikapo jumatano Julai 19 mwaka huu mifugo yote iliyopotea iwe imerejeshwa ndani ya Ranchi hiyo.Waziri Mpina alisema hatua zilizochukuliwa za kuwasimamisha kazi watumishi wawili  kufuatia wizi huo ni njama za kuficha mtandao wa uhalifu huo na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina ili kuunasa mtandao wote uliohusika katika kashfa hiyo.Akitoa taarifa kuhusu kampuni hiyo, Kaimu Meneja wa NARCO, Lutagwelera alisema kwa sasa wataendelea kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo katika kusimamia ulinzi wa rasilimali hizo ili vitendo kama hivyo visitokee tena ili kuongeza uzalishaji mifugo kwenye ranchi hiyo.,

Na Mwandishi Wetu, Siha
AGIZO lililotolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kuhusiana na Kashfa ya Wizi wa ng’ombe 17 wenye thamani ya shilingi milioni 14 katika Ranchi ya Taifa ya West Kilimanjaro limetekelezwa baada ya Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu kukabidhiwa ng’ombe hao baada waliokuwa watumishi wa ranchi hiyo kununua wengine.

Mkuu wa Wilaya ya Siha, Onesmo Buswelu, alisema ng’ombe  amekabidhiwa na Meneja wa Kampuni hiyo, Mbelwa Lutagwelera ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mpina aliyeagiza ngombe kurejeshwa kwenye ranchi na kukataa sababu zilizokuwa zimetolewa kuwa ng’ombe wameibiwa.

“Ni kweli nimepokea leo ng’ombe hao baada ya kurejeshwa kama Mh Waziri alivyoagiza alipotembelea Ranchi hii kwamba mifugo hiyo ipatikane haraka na hatua ziendelee kuchukuliwa kwa wote waliohusika na kashfa hiyo”alisema Buswelu.

Pia Mkuu huyo wa wilaya ameagiza Menejimenti ya NARCO kuajiri walinzi wenye sifa na hasa waliopitia mafunzo kutoka kutoka Jeshi la Akiba ambao wamefundishwa uadilifu na uzalendo wa nchi yao, badala ya kuajiri watu wasiokuwa na sifa.

Buswelu aliwataka watumishi wa ranchi hiyo kusimamia ulinzi wa rasilimali za kampuni hiyo na kujiepusha na vitendo vya kuwa sehemu ya kuhujumu na kushiriki vitendo vya wizi na badala yake wazalishe ng’ombe wengi ili taifa lipate fedha nyingi kutokana na mifugo.

Wakati Waziri Mpina alipotembelea Ranchi hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo aliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata kwa watumishi wote wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) West Kilimanjaro kufuatia kashfa ya kupotea kwenye Mazingira ya kutatanisha ng’ombe 17 wa Serikali waliokuwa wanatunzwa kwenye ranchi hiyo.

Buselu amesema tangu wizi huo ufanywe hakuna taarifa yoyote iliyowasilishwa kwenye Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo jambo linaonesha kuna njama za makusudi zilizowekwa na watumishi hao kuiibia Serikali jambo ambalo halikubaliki.

Hivi karibuni, Waziri wa Mifugo na Uvivi, Luhaga Mpina alipoitembelea wilaya hiyo, alieleza kutokuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Ranchi kuhusiana na kashfa hiyo na kuagiza kuwa ifikapo jumatano Julai 19 mwaka huu mifugo yote iliyopotea iwe imerejeshwa ndani ya Ranchi hiyo.

Waziri Mpina alisema hatua zilizochukuliwa za kuwasimamisha kazi watumishi wawili  kufuatia wizi huo ni njama za kuficha mtandao wa uhalifu huo na kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina ili kuunasa mtandao wote uliohusika katika kashfa hiyo.

Akitoa taarifa kuhusu kampuni hiyo, Kaimu Meneja wa NARCO, Lutagwelera alisema kwa sasa wataendelea kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo katika kusimamia ulinzi wa rasilimali hizo ili vitendo kama hivyo visitokee tena ili kuongeza uzalishaji mifugo kwenye ranchi hiyo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *