Neymar alalamikia ubaguzi

September 14, 2020

Mchezaji nyota  wa  klabu ya  Paris Saint – Germain  amesisitiza kuwa  amekuwa  mhanga wa  ubaguzi  wakati  akiwa  mmoja  kati ya wachezaji watano  kutolewa  nje  kwa  kadi  nyekundu  baada  ya kutokea masumbwi wakati Marseille ikiishinda  PSG katika  mchezo wa  ligi ya Ufaransa  Ligue 1 jana  Jumapili.

Frankreich Fußball PSG- Marseille (Imago Images/PanoramiC/J.B. Autissier)

Vurumai ndani ya uwanja Neymar anamchapa kibao Alvaro

Mchezaji  huyo  nyota  wa  PSG alionekana  kumshutumu Alvaro Gonzalez kwa kumuita  kima, katika wimbi  la  maandishi katika ukurasa wa Twitter baada ya  kutolewa  nje katika  dakika  za nyongeza kwa  kumpiga  kibao mlinzi  wa  marseille kisogoni.”Angalieni kuhusu ubaguzi. Ndio sababu nilimpiga,” Neymar, ambaye  alikuwa  anarejea  uwanjani  kutoka  katika  karantini  ya virusi vya corona, alisema wakati akitoka  uwanjani. Gonzalez baadaye  alikana  kutoa  matamshi  ya  kibaguzi.

Katika  mchezo  huo Marseille  iliishinda  PSG kwa  bao 1-0. Hiki  ni kipigo  cha  pili  kwa  PSG , baada  ya  kupokea  kipigo cha  kwanza kutoka  kwa  Lens siku  ya  Alhamis.

Frankreich Fußball PSG- Marseille (picture-alliance/abaca/D. Niviere)

Bado ubabe kati ya Neymar na Alvaro unaendelea

Neymar alipewa  kadi nyekundu  baada  ya  VAR kuonesha jinsi alivyompiga   kibao kisogoni Gonzalez, wakati mchezaji mwenzake Layvin Kurzawa na  Leandro Paredes pia  walitolewa  nje. Mshambuliaji wa Marseille Dario Benedetto  na  mlinzi Jordan Amavi pia  waliotolewa  nje.

 

Source link

,Mchezaji nyota  wa  klabu ya  Paris Saint – Germain  amesisitiza kuwa  amekuwa  mhanga wa  ubaguzi  wakati  akiwa  mmoja  kati ya…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *