NEC yafanyia maamuzi rufaa (mapingamizi) 55, on September 8, 2020 at 3:00 pm

September 8, 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa rufaa 55 za wagombea Ubunge ambapo, imekubali rufaa 15 za Wagombea Ubunge na kuwarejesha katika orodha ya wagombea na imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa na pia imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera na kusema kuwa zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi rufaa hizo litaendelea, na hivyo Tume itakuwa inatoa uamuzi na kuwajulisha wahusika kwa kadri rufaa hizo zitakuwa zinamalizika kushughulikiwa.Aidha Dkt Mahera ameongeza kuwa Tume hiyo imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa, vilivyowasilishwa ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi na wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa njia ya barua juu ya uamuzi wa Tume kuanzia leo Septemba 8, 2020.Septemba Mosi, 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilitangaza kuanza kusikiliza Rufaa 557 zilizokatwa na wagombea wa ngazi za Ubunge na Udiwani kutoka Majimbo mbalimbali nchini.,

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa uamuzi wa rufaa 55 za wagombea Ubunge ambapo, imekubali rufaa 15 za Wagombea Ubunge na kuwarejesha katika orodha ya wagombea na imekataa rufaa 15 za wagombea ambao hawakuteuliwa na pia imekataa rufaa 25 za kupinga walioteuliwa.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt Wilson Mahera na kusema kuwa zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi rufaa hizo litaendelea, na hivyo Tume itakuwa inatoa uamuzi na kuwajulisha wahusika kwa kadri rufaa hizo zitakuwa zinamalizika kushughulikiwa.

Aidha Dkt Mahera ameongeza kuwa Tume hiyo imechambua vielelezo, nyaraka na maelezo ya warufani na warufaniwa, vilivyowasilishwa ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi na wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa njia ya barua juu ya uamuzi wa Tume kuanzia leo Septemba 8, 2020.

Septemba Mosi, 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ilitangaza kuanza kusikiliza Rufaa 557 zilizokatwa na wagombea wa ngazi za Ubunge na Udiwani kutoka Majimbo mbalimbali nchini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *