Ndugu wa Bilionea Laizer Waanika Mlinzi Alivyouawa

October 6, 2020

 

NDUGU na Meneja wa Bilionea Laizer aitwaye Kiria Laizer amethibitisha taarifa za kifo cha mlinzi wa mgodi wa bilionea huyo kilichotokea usiku wa saa 9 kuamkia siku ya Jumatatu ya Septemba 28, 2020, huko mgodini mahali ambapo alikuwa anafanyia kazi.

 

Kiria Laizer amesema tukio hilo limefanyika ndani ya ukuta wa Mererani ambapo mlinzi huyo alipigwa na kitu chenye ncha kali kichwani  na kwa sasa kesi hiyo ipo mikononi mwa polisi.

 

“Tulienda kwenye eneo la tukio tukamkuta marehemu pembeni mwa hema la kuhifadhia zana, tukamkuta amelala nje na alikuwa tayari ameshapoteza maisha ambapo alikuwa na jeraha kubwa kwenye kichwa;  kwa harakaharaka unaweza kusema amepigwa na kitu chenye ncha kali,” ameeleza Kiria Laizer.

 

“Mwili bado haujazikwa kwa sababu familia ina utaratibu wao ambao wanaendelea nao na wakiwa tayari taratibu za mazishi zitafanyika, kwa sasa hatuna ripoti yoyote ya polisi bali uchunguzi bado unaendelea,” ameongeza.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *